KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TASAF ZANZIBAR
Na Lusungu Helela- UNGUJA Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika kisiwa cha Unguja Zanzibar. Kamati hiyo, imetoa pongezi hizo baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Ukumbi wa Mitihani na Dahalia ya wanafunzi wa kike […]