WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA BARABARA NA ALAMA ZAKE
NGARA Upo umuhimu mkubwa kwa wananchi kuzitunza barabara pamoja na alama za barabarani ili kuzifanya barabara kuwa salama kwa watumiaji wakati wote, imeelezwa. Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilayani Ngara Mkoani Kagera Mhandisi Makoro Magori wakati akielezea mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. […]