SERIKALI KUGHARAMIA MATIBABU KWA MAJERUHI NA MAZISHI YA WANAFUNZI WA AJALI – BAHI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Serikali itagharamia mazishi ya Wanafunzi wawili (2) wa shule ya sekondari Mpalanga Wilayani Bahi waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea jana majira ya saa 5:00 asubuhi katika Kijiji cha Chidilo Wilayani humo. Aidha, Mhe. Senyamule ameahidi kuwa, Serikali itagharamia matibabu ya wanafunzi wote majeruhi31 walioumia katika ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Ajali hiyo imehusisha gari yenye […]