SHUGHULI ZA UHIFADHI ZINAZOFANYWA NA TAWA KALIUA ZINA.FAIDA KUBWA SANA
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dr. Rashid Chuachua amesema shughuli za uhifadhi na Utalii hususani Uwindaji wa Kitalii zinazofanywa na kusimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) zina faida kubwa wilayani humo. Ameyasema hayo Oktoba 24, 2023 katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa jamii iliyofanywa na TAWA wilayani Kaliua. […]