BASHUNGWA AAGIZA KUKAMATWA KWA MKANDARASI ANAYEJENGA DARAJA LA MPIJI CHINI-DAR
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni (OCD), Mohamed Senkondo, kumshikilia Meneja Mradi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group (CRSG), anayetekeleza ujenzi Daraja la Mpiji Chini (mita 140) pamoja na barabara unganishi (km 2.3), ahojiwe ili kuanza kuchukuliwa hatua kwa kuchelewa kuanza ujenzi wa daraja hilo na barabara unganishi. […]