Shakira alishinda tuzo ya mafanikio ya maisha katika Tuzo za Muziki za Video za MTV mapema mwezi huu Mwanamuziki wa pop wa Colombia, Shakira amefunguliwa mashtaka ya kukwepa kulipa kodi kwa mara ya pili na serikali ya Uhispania. Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanadai muimbaji huyo aliilaghai serikali ya Euro milioni 6.7 ($7.1m, £5.8m) mwaka wa […]
SHIRIKA la Taifa la Maendeleo (NDC) limesema ndani ya kipindi cha mwaka mmoja linajivunia maendeleo yake kwa kufanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo imekuwa ikigusa sekta muhimu za kilimo, viwanda, madini, nishati pamoja na miundombinu ya biashara. Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam jMkurugenzi Mtendaji wa NDC, Dkt Nicolaus Shombe wakati akizungumzia mafanikio […]
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mh. Constantine John Kanyasu amewapongeza waandaaji wa Maonesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya Madini na pia kupata nafasi ya kuwa Mgeni mahususi katika kutembelea mabanda mbalimbali yaliyoko katika Maonesho hayo Amesema Maonesho haya yameandaliwa vizuri na washiriki ni wengi na hii inaleta hamasa, hususani ushiriki wa bidhaa […]
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Mh.Mohamed Omary Mchengerwa ameshuhudia utoaji saini wa mkataba wa miradi wa uboreshaji wa miundombinu ya miji ya Tanzania uliofanyika septemba 23 katika ukumbi wa JNICC jijini dar es salaam. Akizungumza katika hafla hiyo waziri Mchengerwa amesema mkataba huo ni wa dola mil 110 ambazo ni zaidi ya shilingi […]
GAVANA wa Benki Kuu (BoT) Emmanuel Tutuba amesema,moja ya majukumu ya Benki hiyo ni pamoja na kushiriki katika masuala ya uchumi ambapo hununua dhahabu kwa ajili ya kutunza akiba za nchi badala ya kutunza kama fedha. Tutuba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la BoT kwenye maonesho ya sita ya kitaifa […]
KAMPUNI ya FEMA MINING AND DRILLING LTD inayojihusisha uchimbaji,ucholongaji na ulipuaji wa madini nchini imeshukuru serikali ya awamu ya sita(6) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu kwa kuwapa fursa na nafasi kampuni za kizawa kufanya kazi katika migodi nchini. Akizungumza hayo katika maonesho ya sita ya kitaifa ya teknolojia […]
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM Tanzania pamoja na kuwa kati ya nchi nne zenye mfumo wa maabara ulitengenezwa Kwa matakwa ya nchi husika,lakini inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu wa Uchunguzi Katika maabara. Hayo yalibainishwa na mkurugenzi wa huduma za maabara wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Dk Danstan shewiyo wakati […]
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Kigoma, Steven Mafiga afanye haraka kuwachunguza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Bi. Zainab Mbunda na Mweka Hazina wa Wilaya hiyo, Bw. Majjid Mabanga ili kubaini ni kwa nini miradi haiendi wakati fedha zilishatolewa kitambo. “Kamanda wa TAKUKURU Mkoa kamilisha hiyo kazi kwa […]