Sasa upungufu wa umeme wabakia 218 MW kutoka 421 MW. Hali ya upatikani umeme nchini imeimarika na sasa upungufu wa umeme umebakia 218 MW. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, tarehe 9 Novemba, 2023 Jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya Wabunge waliotaka kufahamu mpango wa Serikali katika kumaliza changamoto za umeme […]
DKT BITEKO ASEMA NI KIELELEZO CHA USHIRIKIANO WA NCHI HIZO MBILI Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda zimetia saini mkataba mahsusi utakaowezesha kuanza kwa kazi ya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi kutoka Tanzania kwenda Uganda. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dodoma na […]
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema kuwa suala linalohusisha ng’ombe 806, kondoo 420 na mbuzi 100 waliokamatwa Serengeti na kupigwa mnada baada ya Mahakama ya Musoma kutoa hukumu, limeshahitimishwa kimahakama baada ya taratibu zote kukamilika. Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Novemba 9,2023 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja ya Mbunge wa […]
●Yatachimbwa kwa kipindi cha miaka 30 ●Ni mradi wa ushirikiano wa Kampuni mbili ● Bilioni 18.6 zimelipwa kupisha mradi wa Heavy Mineral Sand Kigamboni Serikali kupitia Wizara ya Madini itaanza rasmi uchimbaji wa Madini Adimu yaani _Rare Earth Element_ (REE) kupitia kampuni ya uchimbaji madini ya Mamba ijulikanayo kama _Mamba Minerals Corporation Limited_ (MMCL) yenye […]
Aahidi kuendeleza ushirikiano katika kukuza uchumi Korea Kusini yaahidi kuwekeza zaidi Tanzania Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara kutoka nchini Korea Kusini, Mhe.Ahn Dukgeun ambapo ameeleza kuwa, Tanzania na Korea Kusini zitaendelea kudumisha ushirikiano uliopo katika nyanja za kiuchumi na kijamii ili […]
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo leo Novemba 8,2023 amefanya ziara kwa treni za mjini kutoka stesheni ya Kamata kwenda Pugu kuona adha wanazokumbana nazo abiria. Mhe Albert Chalamila alitumia usafiri huo ili kuweza kuwasikiliza abiria na kuona kero na […]
Mahenge kunufaika na mradi wa madini ya Kinywe Kuboresha sekta ya Maji, Afya na Miundombinu Korea Kusini yaridhishwa na miundombinu ya Reli nchini Tanzania imefungua milango ya uwekezaji katika Sekta ya Madini kwa nchi ya Korea ya Kusini ikiwemo kuendeleza ushirikiano wa kikazi katika kufanikisha utekelezaji wa mikakati ya Vision 2030:MadinI Maisha na Utajiri. Hayo […]
Awapongeza kwa kushusha gharama za uagizaji mafuta Asisitiza EWURA kudhibiti vitendo vya urasimu na rushwa mahali pa kazi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuzingatia maslahi ya Watanzania na maslahi ya nchi katika kazi zao […]
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robertinho) pamoja na kusitisha mkataba wa Kocha wa Viungo Corneille Hategekimana Simba imesema katika kipindi cha mpito kikosi kitakuwa chini ya Kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Selemani Matola huku mchakato wa […]