Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Oktoba 4, 2023 amepokea vifaa tiba toka Shirika la DKT international ambavyo amevielekeza katika Wilaya ya Kigamboni na Ubungo Jijini Dar es Salaam. Akipokea msaada huo wa vifaa tiba RC Chalamila amelishukuru Shirika hilo kwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan […]
> _Atoa shukrani kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumuamini na kumteua._ > _Ahaidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa kutosha._ Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya Chama Cha Mapinduzi (UWT) Ndugu. Jokate Mwegelo amepokelewa rasmi alipowasili katika Ofisi za CCM Makoa Makuu Lumumba Jijini Dar es salaam. […]
Leo Oktoba 4, 2023, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwaย Kassim Majaliwa amekabidhi hundi ya Tshs Milioni 500 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) katika uwanja wa Taifa Benjamin Mkapa jijini Dar-es-salaam. Akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhuย Hassan katika halfa ya […]
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa maelekezo kwa Wizara ya Uchukuzi, Bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi wa ATCL kuhakikisha wanatimiza wajibu wa kusimamia vizuri utoaji huduma za usafiri wa anga ili kuimarisha ushindani Kikanda na Kimataifa na hivyo kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa. Makamu wa […]
*Aruhusu ghorofa lijengwe, wawili wasimamishwa, mmoja arudishwa Wizarani * Dodoma nako awasha moto, 11 wasimamishwa kazi WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Elikana Balandya awasimamishe kazi watumishi wawili wa Jiji la Mwanza huku akiagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa huo arudishwe wizarani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Ameagiza ujenzi […]
*Awataka waanzishe vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi kabla ya 2024 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa miezi mitatu kwa Wakuu wa Mikoa yote nchini ambao bado hawajaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025 wawe wameshaanzisha kabla ya mwaka 2024. Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Viongozi na Watendaji Wakuu wa […]
Tanzania inatarajia kupokea ndege mpya ya abiria aina ya Boing B 737-9 Max ambayo itapokelewa katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julias Nyerere Oktoba 3,2023. Mapokezi hayo yataenda sambamba na uzinduzi wa ndege mbili za mafunzo aina ya Cessna 1725 ambazo zitakabidhiwa kwa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) Hayo yamesemwa Leo na waziri […]
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inaandaa mkakati mpya wa ukusanyaji mapato utakaolenga kuongeza mapato ya Taasisi hiyo mara dufu ya makisio yake ya Mwaka wa fedha 2023/2024. Hayo yamesemwa Leo Oktoba 1, 2023 na Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda katika kikao kazi na wakuu wa Kanda na wakuu wa mapori […]