18 views 44 secs 0 comments

SAMIA SERENGETI MUSIC FESTIVAL KUANDIKA HISTORIA

In BURUDANI
April 19, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amerejesha Tamasha la Serengeti Music Festival na sasa linaitwa Samia Serengeti Music Festival ambalo wasanii wote wakubwa watapanda jukwaa moja, litafungwa jukwaa la kihistoria na Tamasha litafunguliwa na Spika wa Bunge na Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

Tamasha hili ambalo linasimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na BASATA litafanyika tarehe 26 Aprili 2025 katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 Asubuhi mpaka usiku.

Msigwa amesema Tamasha hilo litakuwa na msisimko mkubwa kwa sababu litajumuisha wasanii maarufu wa muziki ambao watapanda jukwaa moja kama vile Diamond, Harmonize, AliKiba, Jaymelody, Zuchu, Rayvanny, Nandi na wasanii wengine wa miziki ya aina zote wa chini na maarufu ambao watapiga nyimbo zao mpya na za zamani.

Moja ya vivutio vikubwa vitakavyokuwepo katika tamasha hili ni ujenzi wa jukwaa la ambalo litafungwa mahsusi kwa matukio ya aina hii. Jukwaa hilo limeundwa na ubunifu wa kisasa wa teknolojia na vifaa vya juu ili kuhakikisha kuwa inatoa mwangaza na sauti bora na muundo wake unajumuisha vipengele vya kisasa na vya kiasilia ikitoa mazingira mazuri kwa wasanii kutumbuiza.

/ Published posts: 1934

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram