13 views 12 secs 0 comments

MALIASILI SC YAIHUKUMU MAHAKAMA 28–18

In MICHEZO
April 19, 2025

 

Na Sixmund Begashe

Timu ya Mpira wa Pete ya Wanawake ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeifunga vikali Timu ya Wanawake ya Mahakama kwa mabao 28 kwa 18 katika mchezo uliochezwa leo kwenye uwanja wa michezo wa VETA, mkoani Singida.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo uliovutia mashabiki wengi, Bi. Getrude Kassara, Mratibu wa Michezo wa Wizara ya Maliasili na Utalii, amesema ushindi huo ni zawadi mahsusi kwa Viongozi na Watumishi wa wizara hiyo, ambayo inaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni.

“Tumejiandaa vizuri sana, hatuna sababu ya kutofanya vizuri. Hiki kichapo tulichokipa timu ya Mahakama, ndicho kitakachozikumba na timu nyingine,” alijigamba Bi. Kassara.

Timu zinazoshiriki mashindano ya mwaka huu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI), mkoani Singida, zinaendelea kuingiwa na hofu zaidi zinapobaini kuwa zinakutana na timu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kutokana na uimara wa wachezaji wa Maliasili Sports Club.

/ Published posts: 1934

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram