15 views 50 secs 0 comments

TADB YATOA GAWIO LA KIHISTORIA LA SHILINGI BILIONI 5.58 KWA SERIKALI

In BIASHARA
April 19, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetangaza gawio la kihistoria la shilingi bilioni 5.58 kwa Serikali ya Tanzania kutoka shilingi milioni 850 zilizotolewa mwaka 2023. Taarifa hiyo imetolewa katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa kwa mwaka wa fedha ulioishia Desemba 31, 2024, uliofanyika makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam.

Ameyasema hayo 17 April 2025 Mwakilishi wa msajili wa hazina Mohammed Nyasama Ameipongeza utendaji wa bank ya tadb na kusisisitiza ni taasisi ya kisera yenye mkakati wa kuleta mapinduzi kwenye Sekta ya kilimo,ikiwemo mifugo na uvuvi Kupitia mikopo na mitaji yenye masharti nafuu.



“Bank imeendelea kufanya vizuri,ikizalisha faida ya shilingi Bilioni 24.7 Kwa mwaka 2024 Ambapo ni ongezeko kubwa ukilinganisha na faida ya mwaka 2023,pamoja na gawio hilo kubwa,bank pia imetoa gawio la shilingi Bilioni 5.58 Kwa serikali”. Amesema Nyasama

Nyasama ametoa salamu za pongezi Katika ofisi ya msajili wa hazina Kwa bodi ya wakurugenzi na wafanyakazi Kwa ujumla wa bank ya tadb kuhakikisha Uwekezaji wa serikali unaendelea kuimarika, taasisi inakuwa imara na huduma zinawafikia wananchi na Tanzania bara na visiwani



Nae Mkurugenzi mwendeshaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege, ameeleza mafanikio ya benki kwa mwaka 2024 ikiwemo ukuaji wa faida kwa 31% na kufikia shingi bilioni 24.kwa mwaka 2024,kutoka shilingi Bilioni 18.8 ya mwaka 2023

Amesema hii imechochewa na ongezeko la utoaji wa mikopo kwenye minyororo ya thamani ya kilimo, mifugo na uvuvi

/ Published posts: 1934

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram