
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Albert Chalamila Amesema hakuna mtu yeyote atakae vuruga amani Katika jiji la dar es salaam
Ameyasema hayo Leo 18 April 2028 mkuu wa mkoa wa dar es salaam Albert Chalamila Amesema Jana tumepewa maelezo kadhaa na Kamanda wa Kanda maalumu ya dar es salaam muliro alitoa maelezo Kwa usalama wa dar es salaam
Amesema Kwa mtu yoyote wa chama chochote Cha siasa taasisi ya dini, mtu binafsi au shirika au Kampuni hakuna hata mmoja atakaevuruga amani ambayo iliyojengwa Katika misingi ya uongozi iliyojengwa Kwa hasa uongozi Bora wa dkt Samia
“Tunafahamu kwamba wapo baadhi ya watu ambao wanamalalamiko Yao wazingatie Sheria wazingatie utaratibu wa namna ya kufikisha Katika taasisi au vyombo vinavyohusika ya maswala ya malalamiko”. Amesema Chalamila
ameendelea kufafanua kuwa Niendelee kuwatoa wasiwasi wafanyabiashara wote na wawekezaji wa mkoa wa dar es salaam kwamba kuazia Sasa mpaka baadae utakapofanyika uchaguzi wa serikali kuu na hata baada ya hapo mkoa wa dar es salaam utaendelea kuwa kivutio Cha amani Katika nchi ya Tanzania afrika mashariki ya kati,afrika nzima duniani kote.