

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Soko la Hisa Dar es salaam DSE limesiani Makubaliano (MOU) na jumiya ya Fintech society Tanzania yenye lenga la kukuza matumizi ya suluhisho za kiteknolojia katika ushirikinw masoko ya mitaji na kuwawezesha watanzania kupata elimu ya Fedha.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Aprili 17 wakati wakusaini Makubaliano hayo , Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Bw. Peter Nalitolela Amesema ushirikiano huo utaangiza katika maeneo mbalimbali ikwemo kusaidia mabadiliko ya kidigitali katika huduma za kifedha na kujenga uwezo kqa vijana na wataalam sekta ya fedha.

“Teknolojia ya Fedha ni teknolojia ambayo imekuwa Kwa Kasi sana Kwa kujitika Kwa Kupitia mitandao ya simu kuwawezesha wadau kupata huduma za kifedha kama vile kufanya malipo kuwekeza kutuma pesa sehemu mbalimbali na kuhifadhi kuunga mkono juhudi za kiserikali za uelimishaji wa kifedha teknohama ni sehemu muhimu sana tunapunguza usumbufu” amesema
Ameongeza kuwa Wao kama soko la Hisa wamekuwa wanafanya jitihada hizo binafsi kupitia mtandao wao wa uwekezaji kwa kushirikiana na wadau qa fedha na kukuza juhudi za kuwafikia wananchi katika kuwekeza soko la Hisa

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Fintech society Tanzania Dr Deniss Mwighusa amesema wamefanya tafiti mbalimbali Kwenye maswala ya teknolojia ya Fedha ni kitu ambacho Kwa kiasi kikubwa sana kinakuwa
” Tunajaribu kuangalia wapi na tunahitaji kufanya nini na tumefanya utafiti Katika maswala ya teknolojia ya Fedha basi Ili kuweza kufanikisha tunafanya vizuri huku tukiangazia Maswala ya Mafunzo na Moja ya maeneo ya Siri sana ambayo tunaelekea kufanya Katika mambo ambayo tutafanya na DSE ” amesema Mwighusa