21 views 49 secs 0 comments

RC CHALAMILA KUWALIPIA NAULI WANA DAR ES SALAAM 200 KUSHIRIKI BETIKA MBEYA TULIA MARATHON

In MICHEZO
April 16, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo April 15,2025 akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa Jezi maalum ya *kushiriki Betika Mbeya Tulia Marathon* ambayo mwaka huu inatarajiwa kufanyika Mei 9 – 10, 2025 Jijini Mbeya.

RC Chalamila ameeleza kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na Tulia Trust Faundation Mkoa huo utaanza amsha amsha ya kujinoa kuelekea Betika Mbeya Tulia Marathon mwezi huu April 19, 2025 kuanzia saa 12:00 Asbh katika eneo la Aghakan hadi Cocobeach.

Aidha kupitia amsha amsha hiyo wale ambao watafanya vizuri katika Marathon hiyo ofisi yake itawagharamia wana Dar es Salaam 200 nauli ya kwenda tu Mbeya ili kushiriki Betika Mbeya Tulia Marathon wakati wa kurudi watajigharamia wenyewe.

Vilevile RC Chalamila amesema kufanya mazoezi ni kuunga Mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh  Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa na athari kubwa katika jamii.

Naye Afisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Betika Bwana Rugambwa Pius amesema wamekuja kumuona mkuu wa Mkoa na kumkabidhi Jezi ya kushiriki Betika Mbeya Tulia Marathon kwa lengo la kumkaribisha yeye binafsi lakini pia wana Dar es Salaam ili waweze kushiriki Marathon hiyo kwa wingi zaidi wakiungana na wakazi wa Mbeya na maeneo mengine ndani ya nchi yetu ya Tanzania.

/ Published posts: 1928

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram