
1. Kupitia nyakati ngumu yaweza kuwa sehemu ya kawaida ya maisha yetu ya kila siku
2. Nyakati ngumu zinaweza kuwa ngumu zaidi kiasi kwamba zikakufanya kulemewa
3. Kulemewa na jambo ni kuwa katika mazingira ambayo mambo yamekuwa magumu, yamefika shingoni, mwanga ulotazamia uone basi ni mwanga hafifu kiasi cha kupoteza nuru
4. Nyakati za kulemewa na mambo unaweza kuhisi kabisa vitu haviendi, hakuna njia kabisa ya kutoka
5. Nyakati hizi mtu anaweza kuona hata uwezo wake wa kutatua mambo umefikia mwisho, kila njia alojaribu haijaleta majibu wala kumpa mwanga
6. Kulemewa kunaweza kumfanya apoteze furaha au hata uchangamfu wake maana kama kuwaza kawaza bila kuona njia inayoweza kumpa kuvuka.
7. Kulemewa kunaweza kuwapeleka wengine hata watafute furaha katika njia zenye hatari zaidi mfano kunywa pombe
8. Kulemewa kunaweza kuwafanya wengine waone tumaini lao la mapambano taa imezimika
9. Nyakati hizi ni nyakati za kukiri na kuhitaji msaada
10. Kulemewa na mambo kunaweza kuwa na nafuu pale unapofikia wakati ambao wazi kabisa unahitaji msaada ili usiendelee kuzama zaidi katika hali mbaya
Kuomba msaada kabla hujalemewa ni mara kumi zaidi