JUA SABABU 69 ZA MWARUBAINI KUWA TIBA MATAIFA YOTE NCHINI

In UCHAMBUZI
March 19, 2025


1. Kwa Waswahili unaitwa Mwarobaini kwa sababu unatibu magonjwa arobaini.


2. Kwa Wahindi unaitwa Duka la Dawa la Kijiji kwa sababu unatibu magonjwa zaidi ya 100.


3. Kuanzia mizizi, magome, matawi, majani, maua mpaka mbegu ni dawa! Ukiupanda unakaa miaka 200!


4. Mti huu upo karibu kila kona ya Dunia. Kwa Tanzania upo mwingi Dodoma!


5. Unaitwa Holy Tree yaani Mti Mtakatifu. Mti wa uzima!


6. Umechoshwa na malaria? Chuma majani yake, kiganja kimoja, chemsha kwa dakika 10, gonga glasi moja asubuhi, glasi moja jioni kwa siku 7, sikilizia.


7. Umechoshwa na kula dawa za maumivu ya mwili na uchovu? Chukua majani matatu ya mwarobaini, tia kwenye maji ya moto, gonga, sikilizia.


8. Umechoshwa na njia hatari za uzazi wa mpango za vijini, majira, P2 na mimba zisizo na mpango? Tumia mafuta ya mwarobaini, sikilizia.


9. India wametangaza rasmi mwarobaini kuwa njia salama ya uzazi wa mpango.


10. Hauna madhara kwa mtumiaji kama ilivyo vipandikizi, vidonge na P2.


11. Haya mafuta sasa unayapataje? Unayapata kwenye mbegu za mwarobaini.


12. Kama huwezi kukamua mwenyewe nenda madukani utayapata.


13. Wazee wa zamani walitumia njia hii katika uzazi wa mpango na watoto walizaliwa kwa mpishano sawia.


14. Yaani kama ni miaka miwili basi ulikuta watoto wote 10 wamepishana miaka miwili miwili na mama yao bado chuma!


15. Siku hizi mama akizaa watoto wawili kwisha habari yako.


16. *Tatizo ya hizi njia za kizungu zinamzeesha mtu kabla ya kuzeeka. Mama aliyezaa mara mbili utadhani kazaa mara 10!


17. Kwa mujibu wa Wanasayansi wa India’s Defence Institute of Physiology and Allied Sciences (DIPAS), mafuta hayo unayopaka kwenye vifaa vya za uzazi kabla ya tendo kuanza.


18. Wanasema yakigusa mbegu za mwanaume zinakufa ndani ya dakika 30.

 
19. Tumieni tu hayana madhara yoyote katika mwili kama vipandikizi na P2.


20. Umechoshwa na fangasi za kila aina mpaka zile za kwenye vidole, kucha, nywele, mdomo na kwa mama mkwe? Chemsha magome ya mwarobaini, gonga, sikilizia!


21. Umechoshwa na matatizo ya kusaga chakula tumboni? Gonga chai ya mwarobaini kisha sikilizia.


22. Umechoshwa na mnuko wa kinywa chako? Kata tawi la mwarobaini, tumia kama mswaki kusugua meno yako, sikilizia!


23. Umechoshwa na ganzi mwilini? Gonga chai ya mwarobaini, sikilizia.


24. Umechoshwa na mlundikano wa sumu mwilini? Chemsha magome ya mwarobaini, gonga halafu sikilizia.


25. Umechoshwa na vipele, chunusi? Tumia sabuni ya mwarobaini, ukiikosa, chemsha majani, oga, sikilizia!


26. Umechoshwa na wadudu wanaozagaa ndani kwako? Choma majani makavu ya mwarobaini, sikilizia!


27. Umechoshwa na kiungulia? Chemsha magome ya mwarobaini, gonga, sikilizia.


28. Umechoshwa na kikohozi? Chemsha magome ya mwarobaini, gonga, sikilizia.


29. Umechoshwa na matatizo ya ngozi? Choma majani jipake, sikilizia!


30. Umechoshwa kubeba minyoo tumboni? Chemsha magome ya mwarobaini, sikilizia.


31. Umechoshwa na maumivu ya tumbo? Chemsha mizizi ya mwarobaini, gonga, sikilizia!


32. Umechoshwa na nywele dhaifu, zinakatikakatika? Tumia mafuta ya mwarobaini, sikilizia!


33. Umechoshwa na pumu? Chemsha magome na mizizi ya mwarobaini, gonga, sikilizia.


34. Umechoshwa na kisukari? Gonga chai ya majani ya mwarobaini, sikilizia.


35. Umechoshwa na UTI isiyopona? Gonga chai ya mizizi ya mwarobaini, sikilizia.


36. Umechoshwa na presha ya kupanda? Chemsha majani ya mwarobaini, gonga, baada ya wiki moja, kapime presha!


37. Umechoshwa na homa za kila siku? Chemsha mizizi ya mwarobaini gonga, sikizia!


38. Umechoshwa na vipodozi vikali sura imekuwa kama chatu? Twanga majani ya mwarobaini, jipake usiku wakati wa kulala, sikilizia!


39. Umechoshwa na mashetani na maluelue ndani ya nyumba yako? Kata jani la mwarobaini, weka mlangoni, habari sikilizia!


40. Umechoshwa na mlundikano wa mafuta mwili na kupumua kwa shida? Gonga chai ya mwarobaini, sikilizia.


41. Umechoshwa na chawa, utitiri, na kupe kwenye kuku wako? Twanga majani ya mwarobaini wamwagia kuku na mabandani, sikilizia.


42. Umechoshwa na harufu mbaya ukeni? Chukua majani ya mwarobaini, chemsha, chuja, acha ipoe, anza kuoshea ukeni asubuhi na jioni kwa siki 6 hadi 14, sikilizia.


43. Umechoshwa na goita? Chemsha mizizi ya mwarobaini kwa dakikia 30, gonga asubuhi na jioni kwa wiki mbili, kisha sikilizia.


44. Umechoshwa na madonda ya tumbo? Chukua majani ya mwarobaini tia kwenye maji ya moto, gonga kwa wiki 2 sikilizia.


45. Umechoshwa na vibarango, vya watoto? Ponda majani ya mwarobaini, kamua, paka yale maji kwenye kibarango, sikilizia.


46. Umechoshwa na saratani ya tezi dume, kongosho, shingo ya uzazi na nyingine kama hizo? Gonga chai ya mwarobaini kila siku asubuhi na jioni mpaka tatizo liishe.


47. Unapenda kula vitu vyenye sukari sana na vinavyoganda kwenye meno kama biskuti? Gonga kikombe kimoja cha chai ya mwarobaini kila mwezi!


48. Una kidonda sehemu yoyote mwilini? Choma majani ya mwarobaini, chukua majivu yake, paka kwenye kidonda, sikilizia!


49. Sasa mpaka hapa unaelewa kwa nini Wahindi wanauita mti huu ni Duka la Dawa la Kijiji.


50. Halafu wanauheshimu sana. Wanajua nguvu ya asili. Asili inaponya.


51. Japo dawa za asili zinatibu slow ila zikitibu zimetibu.


52. Tofauti na dawa za kemikali zinatibu haraka na kuacha madhara makubwa. Zinaitwa tumia na kesho rudi!


53. Wahindi wanakwambia mwarobaini una nguvu za kiroho ndani yake. Mungu wa wahindu aitwaye Devas anaishi katika mti huo!


54. *Ndiyo maana mtoto akizaliwa wanamlaza kwenye majani ya mwarobaini avune baraka za Mungu kupitia mti huo!*.


55. Hata kivuli cha mti wa mwarobaini ni salama sana. Hakina wadudu chini. Harufu ya mwarobaini hufukuza wadudu.


56. Jenga utaratibu wa kunywa walau glasi moja ya maji ya mwarobaini kila baada ya miezi sita. Nakwambia hutokutana na malaria maishani.


57. Maua na majani machanga ya mwarobaini ni mboga, chuma pika, gonga, inaitwa mboga dawa!


58. Leo wahindi wanatikisa kwa tiba duniani. Wanajua nguvu ya asili. Asili inaponya.


59. Wametengeneza dawa za kumeza, dawa za meno, sabuni, losheni  na majani ya chai kutokana na mwarobaini.


60. Sisi bado tunaona aibu kutumia mitishamba. Tunaita ushirikina.


61. Tumefyeka miti dawa na kupanda miti kichaa, miti inayokausha ardhi na kuleta ukame!


62. *Angalizo!* Tofauti na miti mingi, mwarobaini haufanyi kazi ya kuua vijidudu tu, wenyewe unaua mpaka kizazi cha vijidudu.


63. Pale inapotumika iwe kwa binadamu, mimea au wanyama hufanya kazi za  kuua kizazi chake.


64. Kwa hiyo mtu anayetumia sana mwarobaini kwa kunywa anaweza poteza kizazi pia. Hili ukalichukue.


65. Ingawa toka mwarobaini umeanza kutumika kama dawa kwa miaka zaidi ya 4000 na hakuna majanga yaliyowahi kuripotiwa inashauriwa kuwa na tahadhari kama ilivyo kwa dawa za kisasa.


66. Umakini unaotakiwa katika matumizi ya dawa za kizungu unatakiwa pia katika dawa zetu za asili.


67. Watoto wadogo wanywe mwarubaini chini ya uangalizi wa madaktari bobevu.


68. Usinywe mwarobaini kwa wiki sita mfululizo maana unaweza kuharibu maini na figo zako.


69. Kama unataka kumroga mtu ili maisha yake yawe machungu basi unatumia mwarobaini. Unarogaje? Sijui!

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram