
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kudumu miaka 130 huku ukiwa unafanyiwa marekebisho kila baada ya miaka 10.
Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo walipotembelea mradi wa uwanja huo kwa ajili ya kujionea maendeleo yake.
Mhe. Mwinjuma ameongeza kuwa mradi huo umefikia asilimia 33 na utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 32,000 utakapokamilika ifikapo Juni 2026.









