8 views 2 mins 0 comments

RC CHALAMILA AZINDUA OFISI YA MACHINGA-DSM

In KITAIFA
March 14, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-Amshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutoa pesa zilizowezesha ujenzi wa ofisi hiyo.

-Awataka machinga na Bodaboda kuitumia ofisi hiyo kuleta matokeo chanya.

-Arudisha tabasamu la Bi Beatrice aliyekumbwa na sakata la kuuzwa nyumba yake

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 13, 2025 amezindua ofisi ya Machinga Mkoa ambayo imejengwa katika eneo la TBA, Kata ya Ndugumbi Magomeni Kota Wilaya ya Kinondoni.

Akifungua ofisi hiyo ya kisasa RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa ya ujenzi wa ofisi ya machinga na mradi mingine inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo ambapo amesema furaha ya Rais Samia ni kuona watanzania wanakuwa wanufaika chanya wa miradi hiyo ili kuwa na jamii yenye ustawi.

RCย  Chalamila amesema ofisi aliyoizindua itatumiwa na machinga Mkoa pamoja na Bodaboda Mkoa ambapo ameyataka makundi hayo kuitumia ofisi hiyo vizuri ili kuweza kuleta matokeo chanya

Naye Bi Zubeda Masoud akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Dkt Toba Nguvila amesema ujenzi wa ofisi hiyo ya machinga ni maagizo ya Rais Samia kuwa kila Mkoa uwe na ofisi ya Machinga ambapo alitoa pesa shilingi milioni 10 kupitia OR-TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo ambayo imezinduliwa leo.

Vilevile kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amemshukuru Rais Dkt Samia kwa ujenzi wa ofisi hiyo na kuahidi kama Wilaya kumalizia baadhi ya vitu vichache ikiwemo samani na kompyuta ili waweze kufanya kazi zao kisasa zaidi.

Hata hivyo viongozi wa Machinga na Bodaboda kwa nyakatiย  tofauti wamemshukuru Mhe Rais kwa kulitambua kundi hilo muhimu na wao wako bega kwa bega naye lakini ombi lao ofisi hizo zijengwe pia katika ngazi za Wilaya zote za Mkoa huo

Sambamba na hilo RC Chalamila amerudisha tabasamu kwa Bi Beatrice William ambaye amekumbwa na sakata la kuuzwa nyumba yake ambapo amemhakikishia ofisi yake kwa kushirikiana na TLS imeshaweka pingamizi la kimahakama hivyo nyumba hiyo haitauzwa kwa sasa pia ameongoza changizo kwa ajiri ya kumfariji mama huyo ambapo yeye binafsi ametoa milioni moja huku watu wengine wakijitokeza kwa wingi kumchangia.

/ Published posts: 1816

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram