
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe mkoani Mbeya kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu kuanzia Machi 13 hadi 16, 2025 mkoani Songwe.
Uwanjani hapo Makamu Mwenyekiti Wasira alilakiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo.


