
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) yaonesha tafiti ya gesi ASILIA imetumika Kwa Kiasi kikubwa Katika usafirishaji na usafiri
Hayo yameelezwa na Afisa Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano kutoka Ewura, Wilfred Mwakalosi wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti waliofanya katika Kongamano la 11 na Maonesho ya Petroli Nchi Wanachama Afrika Mashariki (EAPCE’25).

“utafiti huo umefanyika kuanzia Septemba 2024 hadi Januari 2025, ambapo ulilenga kuchunguza kutakuwa na faida gani za kiuchumi na kijamii iwapo nchi itaamua kutumia kwa kiwango kikubwa gesi asilia kwenye usafiri na usafirishaji”Amesema Mwakalosi
“Ni Utafiti ambao upo katika kundi la namna ambavyo Nchi za Afrika Mashariki zinaweza zikachanganya vyanzo vya nishati ili kuleta unafuu. Tulikuwa tunataka kuangalia hivyo kwasababu kama mnavyofahamu sekta ya usafiri ndio kila kitu, usafiri gharama yake ikiwa kubwa hata mbolea kufika Songea itakuwa gharama kubwa, hata mafuta yenyewe kuyasafirisha gharama yake itakuwa kubwa.

“Bei za bidhaa mbalimbali jinsi zinavyokuwa kubwa zinakwenda kuathiri kwenye mfumuko wa bei. Kwahiyo tulikuwa tunaangalia je kama gesi asilia ambayo inapatikana nchini, itatumika kwenye usafiri na usafirishaji itaweza ikawa na manufaa gani kwa kuzingatia gharama yake iko chini sana,” amesema Mwakalosi
Amebainisha kuwa matokeo ya utafiti yameonesha kuwa endapo gesi asilia itatumika hasa kwenye usafiri wa umma mfano malori, mabasi, daladala ni dhahiri kuwa gharama za usafirishaji zitakuwa chini.UTAFITI uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) umeonesha kuwa endapo gesi asilia itatumika kwa kiasi kikubwa kwenye usafiri na usafirishaji gharama za maisha zitapungua.