
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
GSM Foundation na Hospital ya CCBRT leo wamesaini makubaliano ya ushirikiano ambapo GSM Foundation inaongoza kampeni ya kuchangisha kiasi cha milioni 588,734 ,880 za kitanzania kwaajili ya matibabu ya watoto 400 waliozaliwa na tatizo la miguu kifundo (clubfoot) ambapo wanapokea matibabu katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam

Akizungumza wakati wa Hafla ya utiaji saini iliyofabyika Hospitali ya CCBRT Msasani Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa GSM Foundation Faith Sugu alisema kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na CCBRT ,Klabu ya soka ya Yanga na Wizara ya Afya imeandaa hafla yakuchangisha fedha kupitia Iftar maalum katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na tukio hilo litafanyika katika ukumbi wa the Super Dome Masaki Dar es Salaam 14 Machi 2025 kuanzia saa 11:00 Jioni hadi saa 2:00 Usiku
“Sisi kama @gsmfoundationtz tunapenda kuwashukuru wadau wetu wakubwa @ccbrtofficial kwani tumekuwa na mahusiano mazuri sana.

Tumeanza mazungumzo tokea mwaka jana ambapo walileta maombi kwetu kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye mguu kifundo. Hivyo kwa kushirikiana na Young Africans tukaamua kuchangisha fedha” Faith Gugu, Mkurugenzi GSM Foundation

Na Kwa upande wake Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisema kuwa kama klabu ya mpira wa miguu wanao wajibu wa kusaidia kujenga jamii bora na yenye ustawi zaidi huku akiwakaribisha wadau wengine kutoka sekta mbalimbali ikiwemo pia michezo wajitokeze kwa wingi kusaidia watoto hao ambao baadae huenda wakaja kutimiza ndoto zao ikiwemo kuwa wachezaji wakubwa wa mpira wa miguu akimtolea mfano aliyewahi kua kiungo wa Liverpool na timu ya Taifa ya uingereza Steven Gerald