
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
DAR ES SALAAM:
KATIBU Tawala mkoa wa Dar es Salaam Dk. Toba Nguvila amesema katika kuhakikisha usalama katika soko la Kariakoo, tayari serikali kupitia Halmashauri ya jiji hilo imeshasaini mkataba na Wakalawa Ufundi na Umeme Tanzania TAMESA kwaajili ya ufungaji wa kamera 40 za ulinzi ( CCTV Camera) kazi itakayoanza Machi Mosi mwaka huu zenye thamani ya Shilingi milioni 514.
Amesema hii itasaidia katika kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.
Amesema Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) pia limeanza utaratibu wa kubadilisha nguzo za umeme kutoka za miti hadi za zege na kuweka nguzo za ili kuhakikisha linaboresha miundombinu ya umeme jambo ambalo limefikia asilimia 90 ya ukamilikaji wake.
Amesema pia kwa kushirikiana na Halmashauri ya jiji, Wakala wa Barabara Vijijini ( TARURA), wanatarajia kufunga taa 730 katika maeneo ya Kariakoo ili kuhakikisha mwanga kwa masaa yote 24.
Aidha ameninisha kuwa Jeshi la Polis pia limejipanga katika kuhakikisha usalama unakuwepo muda wote.