132 views 2 mins 0 comments

WAZIRI MAJALIWA KUWA MGENI RASMI TUZO ZA VALENTINE EVE PATRIOTIC AWARDS

In KITAIFA
January 31, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

waziri mkuu kasim majaliwa kuwa mgeni rasmi Katika siku ya “VALENTINE EVE PATRIOTIC AWARDS 2025″” Itakayofanyika Katika ukumbi wa hayyat Regency Tarehe 13 jijini dar es salaam.

Siku hiyo watakutana wataalumu wa saiko-sosholojia  Ambapo watazungumzia maswala ya ugonjwa wa kuambukiza ambao unasadikika ni hatari sana Kwa jamii na ugonjwa huo ni CHUKI

Amesema kuwa chuki hasi Iko chini ya kategoria ya hisia,kama hisia zote zilivyo,chuki yaweza kuwa chanya au hasi kulingana na jinsia inavyotumiwa Amesema Kwa mfano,kuchukia rushwa au vurugu ni matumizi mazuri,huku ubaguzi wa rangi,kutovumiliana Katika tofauti za amani au unyanyasaji wa kijinsia ni chuki hasi



Akizungumza na waandishi wa habari Leo Januari 13 2025  Mkurugenzi Mtendaji wa Family Vibes Foundation, Dk Mayrose Majinge alisema lengo la tunzo hizo ni kuelimisha jamii ya watu mashuhuri  ambao wameonyesha  uzalendo kwa nchi yao

Alisema kuwa Dunia kwa sasa imetawaliwa na ugonjwa wa ‘chuki’ ambao umekuwa hatari zaidi ya magonjwa yote.

“Tunzo hizi pia zina lengo la kuhamasisha uzalendo kwa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na madhara ya chuki hasi nchini” alisema.

Alisema kuwa suala la mmomonyoko wa maadili na madhara ya chuki hasi vimekuwa vikiathiri maisha ya kila siku na kuondoa ladha ya maisha kwa muda mrefu  bila kupata muafaka wake.


  “Kuna gonjwa la hatari sana linaitwa chuki, kwa macho huwezi kujua hathari zake, na hii yote inatokana na kukosa kipato.” Alisema.

Katika kuandaa mbinu ya kuwapata watu washuhuri tuliamua kuandaa siku hii maalumu ambayo inaendana na siku ya wapendao Ili kuwapa somo watu mashuhuri.

/ Published posts: 1695

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram