Home > KITAIFA 37 views 5 secs 0 comments MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA YAFANYIKA JIJINI DODOMA In KITAIFA January 25, 2025 Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakishiriki maandamano ya Wiki ya Sheria kabla ya uzinduzi wa maadhimisho hayo yanayoendelea Jijini Dodoma. Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Jijini Dodoma. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na watumishi na wadau wa Mahakama ya Tanzania wakati akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Jijini Dodoma. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Hamis Juma akitoa salamu za Mahakama kwa watumishi na wadau wa Mahakama wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Jijini Dodoma.