Na MWANDISHI WETU
-DODOMA
NI Samia tena urais 2025-2030. Ndivyo unavyoweza kusema hasa baada wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi kumpitisha kuwa mgombea wa urais wa chama hicho tawala.
Hatua hiyo ya kufikia uamuzi wa kutaka kuwapitisha kuwa wagombea wa urais kwa upande wa Bara na Zanzibar kama njia muhimu ya kukifanya chama kijipange na ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Baada ya hoja hiyo iliyowasilishwa na na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa ambapo aliungwa mkono na wajumbe wengine na kulazimika kuandaliwa azimio ambalo liliitaka Halmaahauri Kuu ya Taifa ya CCM kwenda kukutana na kuandaa azimio ambalo lilikubaliwa na kisha kufuta utaratibu ikiwamo kuandaliwa kwa vikao na kisha mkutano Mkuu kulazimika kupiga kura.
Kutokana na hali hiyo ilimlazimu Rais Dkt. Samia kutoka ukumbini na kumuachiwa kiti Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye baada ya kukamilisha mchakato huo wa upigaji kura uliosimamiwa na Mwenyekiti wake Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
Hata hivyo baada ya kukamilika kwa mchakato huo, Dkt Mwinyi alitangaza matokeo na kumtangaza Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata kura 1924 ambazo ni sawa na asiliamia 100 ambapo hakukuwa na kura ya Hapana wala iliyoharibika.
“Mheshimiwa Mwenyekiti (Samia) ninapenda kwa kukupa taarifa kuwa Mkutano Mkuu wa Chama umekamilisha mchakato wake kama ifuatavyo, jumla ya kura zote 1924 hakuna kura iliyoharibika waka ya Hapana. Hivyo kwa matokeo haya Mkutano Mkuu umemchagua Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100,”alisema Dkt Mwinyi na kisha kurudisha kikao kwa Rais Samia.
MGOMBEA MWENZA
Baada ya kukamilisha hatua hiyo, akiendesha kikao hicho Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, aliwashukuru wajumbe kwa kuendelea kumuamini huku akiwaomba wawe na utulivu na kuwataka wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwenda kwenye kikao na kujadili suala la nani mgombea mwenza.
Kikao hicho cha Kamati Kuu, kilikwenda kufanyika kwa muda wa dakika 40 na baada ya hapo walirejea ukumbini ndipo alipoingia Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Samia.
“Tumekamilisha mchakato awali huku nyuma alikuja kuniambia Dkt. Philip Mpango kuwa anahitaji kupumzika ili aweze kuishi zaidi, kwani sasa ana miaka 68 na mama yake ana aliishi miaka 86 na yeye anataka kuishi zaidi ya hapo. Alipoona hivyo sijamjibu wiki iliyopita aliniandikia barua nayo sijamjibu na hili nimewashirikisha kaka zangu hawa watatu ( Jakaya Kikwete, Dkt Ali Mohamed Shein na Dkt Aman Karume.
“Baada ya majadiliano ya kina ya nani anaweza kuwa mgombea mwenza, nao waliweza kujadili na leo (jana) tumejadili kwenye kamati kuu na kufikia maamuzi ya kumleta kwenu kijana wetu Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza. Na pia mtajiuliza sasa kazi zitakuwa ila ataendelea kubaki kuwa Katibu Mkuu na tutaenda kwenye nginjanginja na ataoanga mipango ya namna gani ya kushinda.
“Pamoja nae pia tutaendelea kuwa na Dkt. Mpango kwa kuwa ndiye Makamu wetu wa Rais hadi pale tutakapomaliza naye,” alisema Rais Samia
HALI ILIVYOKUWA
Azimio hilo limepitishuwa jana na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho uliofanyika Mjini Dodoma ambapo wajumbe 1978 wa mkutano huo wamepitisha jina Rais Samia kugombea urais kwa tiketi ya Chama hicho bila kuathiri katiba ya chama cha Mapinduzi.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM*, Mkutano Mkuu una mamlaka ya kufanya maamuzi hayo.Kulingana na Katiba ya CCM, Ibara ya 8(2)(a) inasema:-Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi una mamlaka ya kumteua mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Sehemu ya maelezo yaliyoko katika Azimio hilo yalikuwa yanasema hivi;”Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tukiwa tumekutana jijini Dodoma tarehe 18-19 Januari 2025, tunapitisha azimio hili kwa kauli moja:
Kumteua Mwenyekiti Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.“`
Hivyo baada ya kusomwa Azimio hilo ndipo wajumbe 1978 wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wamepitisha jina la Rais Dk.Samia kugombe nagasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CCM*, Mkutano Mkuu una mamlaka ya kufanya maamuzi haya. Kulingana na Katiba ya CCM, *Ibara ya 8(2)(a)* inasema:-
Hivyo Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi una mamlaka ya kumteua mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu kupitisha Azimio hilo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliuliza kama kuna mjumbe ambaye hayuko pamoja na Azimio hilo lakini hakuna aliyejitokeza ,hivyo Azimio limepita kwa kauli moja.
Awali kabla ya kuandaliwa kwa Azimio na kupitisha jina la Rais Samia kugombea Urais wajumbe wa mkutano huo akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Adam Kimbisa alitoa hoja katika mkutano huo kuridhia kupitisha jina la Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na jina la Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi kugombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Hoja hiyo ilipata kuungwa mkono na wajumbe wengine mbalimbali wote walitoa ombi kwa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Kamati Kuu kukubali maombi ya wajumbe wa mkutano mkuu ambao kwa mujibu wa Katiba unayo maamuzi yote ya kupendekeza jina la mgombea