20 views 3 mins 0 comments

SERIKALI YAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZINATOKANA NA MVUA  KWENYE MIUNDOMBINU YA USAFIRI  WA TRENI YA MWENDOKASI (SGR).

In KITAIFA
January 16, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, amesema kuwa serikali inajizatiti kutatua changamoto zinazotokana na mvua katika usafiri wa treni za Mwendokasi (SGR). Kadogosa ameeleza kuwa mvua kubwa inayoendelea kunyesha inasababisha maji kuingia katika sehemu ambazo ziliharibiwa na wahalifu, hivyo kusababisha hitilafu katika miundombinu hali iliyopelekea kusimamisha  kwa treni kwa masaa 6 hadi 7 njiani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kadogosa amesemakuwa serikali imejipanga kurekebisha maeneo yote yenye changamoto ili kuhakikisha usafiri wa treni unakuwa salama na haukwami njiani huku  akishukuru  Jeshi la Wananchi kwa kudhibiti wizi wa mitambo ya reli na kusema kuwa sasa hali ya usalama imeimarika.

Kadogosa aliongeza kuwa idadi ya abiria wanaosafiri kwa treni ya SGR imeongezeka, ambapo takribani watu milioni 1.4 wamesafiri katika kipindi cha miezi minne, na kila siku watu kati ya 5,000 hadi 10,000 hutumia treni za Mwendokasi.



Aidha Kadogosa amethibitisha kuwa Shirika la reli nchini Tanzania TRC kwa kushirikiana na jeshi la polisi  linaendelea Kudhibiti  uhalifu wa miundombinu ya reli ya kisasa   na Changamoto Zinazotokana na mvua  kwenye miundombinu ya usafiri  Wa treni hiyo.


amesema kuwa Kutokana na changamoto zilizojitokeza katika shirika letu kwa sasa vitendo vya uhalifu vimepungua kwa kiasi kikubwa zaidi hivyo  tunaenda kumaliza changamoto hiyo  katika usafiri wa treni za Mwendokasi (SGR).


“Nitoe pongezi kwa serikali kuweza kutumia usafiri wetu wa treni kwani zaidi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi CCM, Wasanii mbalimbali na viongozi wa chama hicho kutoka Zanzibar,   Lindi, na Mtwara lengo ikiwa ni kwenda kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kwenda kufanyika mkoani Dodoma tarehe 17,18.


Aidha Kadogosa ameongeza  kuwa  kipindi cha  mvua  zinazonyesha inapelekea maji kuingia katika sehemu ambazo ziliharibiwa na wahalifu, hivyo kusababisha hitilafu ya  miundombinu  kusimama kwa treni kwa masaa 6 hadi 7 njiani” Amesema Mkurugenzi kadogosa.



Vilevile Tunaendelea kutatua  changamoto kwenye maeneo ya miundombinu ili kwenda  kuhakikisha usafiri wa treni unakuwa salama zaidi kwa abiria wote.

 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya kisarawe Mhe.Petro Magoti ametoa pongezi kwa serikali kwa kuweza kutumia usafiri wa treni hiyo kuelekea kwenye mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika mkoani dodoma mwaka huu.



Takribani ya wajumbe ambao wanaelekea kwenye mkutano huo na wasanii ni chachu ya kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi katika kutumia usafiri huo pia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anahakikisha wananchi wake wanatumia usafiri huo wa haraka.

/ Published posts: 1642

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram