17 views 5 mins 0 comments

Mapinduzi ya Miaka 61 ya Zanzibar na Ukuaji wa Sekta ya Bima visiwani humo

In BIASHARA
January 12, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 sheria ya bima sura ya 394. Pamoja na majukumu mengine imepewa mamlaka ya kuratibu maswala yote ya kisera kuhusu bima ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ofisi zake za Makao makuu ni Dodoma lakini pia ina Ofisi ndogo Dar es Salaam na Zanzibar.

TIRA ina majukumu mbalimbali yakiwemo kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima,kuandaa na kutoa miongozo kwa watoa huduma za bima, kusimamia soko la bima nchini, kutoa elimu ya bima, kulinda haki za wateja wa bima, na kuishauri serikali kuhusu masuala ya bima.

Kwenye Maadhimisho haya ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar, TIRA inashiriki Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara visiwani Zanzibar katika viwanja vya Fumba Dimani kuanzia tarehe 1 Januari 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 15 Januari, na leo hii Januari 12, 2025 ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Mapinduzi TIRA inawakilishwa na Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware, Naibu Kamishna wa Bima Bi. Khadija Said na Meneja wa Kanda ya Pemba Bw. Sharifu Hamadi huko Visiwani Pemba ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Saluhu Hassan.

Kupitia Ofisi ya Zanzibar iliyopo Unguja ambapo pia ndipo ilipo ofisi ya Naibu Kamishna wa Bima Tanzania, imeweza kufanikisha mambo mbalimbali yanayoashiria ukuaji wa soko la bima visiwani humo.

Kuimarishwa kwa mifumo ya bima TIRA Zanzibar imeweza kuboresha mifumo yake ambapo imeongeza urahisi katika usajili kwa watoa huduma lakini pia mifumo hiyo inaisaidia Mamlaka kuhakikisha watoa huduma wanalipa ada zao kwa wakati na hata kuarifiwa kutozwa faini na adhabu nyingine pale wanapokiuka taratibu.

Kufunguliwa kwa ofisi ya TIRA Pemba Lengo la Mamlaka ni kuhakikisha idadi kubwa ya watanzania wanajua kuhusu bima na kutumia bidhaa hizo, katika Uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima, Kamishna wa Bima Tanzania alibainisha,

“Njia ya mafanikio katika sekta hii ni kuendelea kuwa na ongezeko la asilimia 15% kwa mwaka la watanzania wanaotumia huduma za bima ili kuweza kufikia lengo la asililimia 50% la ongezeko la watanzania wanaotunia huduma za bima ifikapo mwaka 2050
Kwa kuzingatia hilo Mamlaka ilifungua ofisi Pemba ikiwa na lengo la kupeleka elimu na kukuza uelewa visiwani humo,

“Uelewa wa bima hapa Pemba unaongezeka siku hadi siku na wananchi wamekuwa na mwamko wa kutaka kufahamu namna bima inavyoweza kuwasaidia wakati wa majanga na fursa wanazoweza kuzitumia katika sekta hii  kuongeza kipato chao” anasema Meneja awa TIRA Pemba Bw. Sharif Hamad.

Ongezeko la watoa huduma za bima Huduma za bima Zanzibar ni rahisi kuzipata kutokana na ongezeko la watoa huduma hao, “Kwa sasa ni rahisi kupata huduma mbalimbali za bima kutokana na ongezeko la kampuni hizi hapa Unguja” anaeleza Meneja TIRA kanda ya Unguja Bi. Awanje Matenda.

Katika taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa mwaka 2023 ilieleza ongezeko la Ada za Bima (Gross Premiums Written – GPW) ambazo  zimepanda kwa asilimia 7.4 hadi kufikia TZS trilioni 1.24, kutoka TZS trilioni 1.17, watoa huduma za bima wameongezeka kwa asilimia 34, na kufikia 1,549 ikilinganishwa na 1,164 mwaka uliopita.

Aidha, madai ya bima yaliyolipwa yameongezeka kwa asilimia 25.5, hadi kufikia TZS bilioni 488.2 kutoka TZS bilioni 389.
Kiwango cha mali za bima kimeongezeka kutoka TZS trilioni 1.7 hadi kufikia TZS trilioni 2.15  huku uwekezaji pia ukiongezeka hadi  TZS trilioni .1.27 kutoka TZS trilioni  1.17.

Fursa za ajira zimeongezeka kwa asilimia 34.1, ambapo jumla ya ajira 5,595 zimerekodiwa mwaka 2023. Aidha, kiwango cha ubakizaji wa bima za kawaida (general insurance retention) kimeongezeka kutoka asilimia 49.4 hadi asilimia 55.5 huku kiwango cha ubakizaji wa bima za maisha kikiwa ni asilimia nah ii ni kwa Tanzania bara na visiwani.

Ongezeko la Utoaji Elimu, Ofisi ya Mamlaka Zanzibar, imeongeza ushiriki wake katika maonesho kama, Siku ya Bima Zanzibar na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ambapo   Mamlaka inatoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea, pia kupitia ushiriki katika vyombo vya habari kama Televisheni, radio na magazeti wakazi wa Zanzibar hufikiwa katika utoaji elimu.

TIRA inashiriki Maonesho haya ya 11 ya Kimataifa ya Biashara kama njia ya kukutana na wadau wake mbalimbali, kutoa elimu na kusikiliza changamoto mbalimbali za kibima ambazo zinapatiwa majibu ya moja kwa moja.

#TIRA KWA SOKO SALAMA LA BIMA

/ Published posts: 1633

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram