19 views 3 mins 0 comments

WATAKAOHUSIKA KUDHOOFISHA JITIHADA ZA SERIKALI PORI LA AKIBA KILOMBERO KUSHUGHULIKIWA : Mhe. Dunstan Kyobya

In KITAIFA
January 04, 2025



๐Ÿ“ Msako mkali wa “Matapeli” kufanyika

Na Beatus Maganja, Kilombero.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amesema Serikali haitawafumbia macho watu watakaohusika kudhoofisha jitihada za kulinda na kuhifadhi Pori la Akiba Kilomberoย ย  ambalo ni mahsusi Kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji, misitu na wanyamapori hususani upatikanaji wa maji Kwa ajili ya uzalishaji wa umeme katika mradi wa kimkakati wa Bwawa la Mwl. Nyerere.

Akizungumzia umuhimu wa kuhifadhi Hifadhi hiyo Januari 03, 2024 wilayani humo, Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amekemea vikali tabia ya watu wachache wanaowalaghai wananchi kulima na kuchunga mifugo ndani ya Hifadhiย  pamoja na kuwauzia maeneo Kwa ajili ya kilimo.

“Imetokea tabia ya watu kwenda kuwashawishi wananchi kwamba maeneo ya hifadhi yanaruhusiwa kulima na kuchunga mifugo, nasema maeneo ya hifadhi hayaruhusiwi kwa shughuli zozote za kibinadamu isipokuwa zile zinazoruhusiwa kisheria” amesema Wakili Kyobya

“Lakini kuna wengine wanawatapeli wananchi Kwa kuwauzia maeneo ndani ya Hifadhi, nimuombe OCD (Mkuu wa Polisi Wilaya)ย  pamoja na Kamati ya usalama ya wilaya kuendelea kufuatilia kwa ukaribu na wale wote watakaobainika wanawadanganya wananchi, wanawalaghai, wanawatapeli Kwa njia moja ama nyingine tutachukua hatua” amesisitiza Mhe. Kyobya.

Aidha Mhe. Wakili Kyobya ametoa wito Kwa viongozi wa Wilaya yake kuongeza ulinzi katika Pori la Akiba Kilombero naย  kuweka utaratibu mzuri wa kuwapokea wananchi wanaohama kutoka ndani ya Hifadhi hiyoย  hasa katika maeneo yaliyo pembezoni mwa Hifadhi kama vile Mofu, Idete, Mawala, Chombe na Mgeta,

Maeneo mengine aliyoyataja ni pamoja na Chita, kalengakyelu,Chisanoย  Ching’anda,Mlimba, Utengule na mengine yanayozunguka hifadhi huku akisisitiza kuwa imani na niaย  nzuri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan isiharibiwe na watu wachache.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba Jamal Idrisaย  Abdul amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kulipandisha hadhi Pori la Akiba Kilombero na kusisitiza kuwa Kazi iliyobaki ni kuhakikisha Halmashauri Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA wanailinda na kuihifadhi Hifadhi hiyo sambamba na kurejesha uasili wake.

Mkurugenzi huyo amesema mpaka sasa Kazi kubwa wanayoendelea nayo ni kuhakikisha wananchi hawaendelezi shughuli za kibinadamu katika Hifadhi hiyo.

Kwa upande wake Kamanda wa Pori la Akiba Kilombero Bigilamungu Kagoma amesema tangu Hifadhi hiyo ipandishwe hadhi TAWA imeendelea na zoezi la uwekajiย  vigingi ili kuifanya mipaka ya Hifadhi kuonekanaย  na kutambulika vizuri na wananchi ambapo mpaka sasa zaidi ya vigingi 1,100 tayari vimekwisha wekwa.

/ Published posts: 1625

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram