9 views 2 mins 0 comments

BILIONI 18 ZATUMIKA KUNUNULIA VIFAA VYA TEHAMA KWA AJILI YA ELIMU SEKONDARI

In KITAIFA
December 19, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchemgerwa amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa matumizi ya TEHAMA katika ujifunzaji na kujenga umahiri uliokusudiwa kwenye Mitaala kwa wanafunzi wa Sekondari, katika kipindi cha mwaka 2023/2024, Serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 18 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya TEHAMA, ambapo kupitia Programu ya SEQUIP, Shule za Sekondari 1,500 zinatarajiwa kunufaika.



Akizungumza leo Desemba 18, 2024 kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa Shule za Sekondari nchini iliyofanyika katika Shule Maalum ya Wasichana ya Sayansi ya Mkoa wa Dar es salaam iliyopo Manispaa ya Ubungo, Mhe. Mchengerwa amesema vifaa hivyo vinalenga kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa njia ya kisasa kwa kutumia na kujifunza TEHAMA ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia Duniani.


Amesema matumizi ya vifaa vya TEHAMA ni moja ya afua na viashiria vya utekelezaji wa mradi wa SEQUIP inayolenga kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kupitia TEHAMA katika Shule za Sekondari.

Kupitia utekelezaji wa mradi wa SEQUIP jumla ya Shule za Sekondari 1,500 zinatarajiwa kunufaika kwa kupata vifaa vya TEHAMA. Kwa leo hapa tunatoa vifaa kwa shule 231 ambazo ni sehemu  ya shule hizo 1,500 zitakazonufaika na mpango huu.


 
Katika kufanikisha azima hii, Serikali ilianza kutoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA na huduma ndongondogo ya vifaa hivyo kwa walimu 3,132 wa Shule za Sekondari.
 
Utoaji wa mafunzo kwa walimu hawa unalenga kuhakikisha walimu wamejengewa uwezo katika kutunza Vifaa vilivyonunuliwa, kutumia vifaa kwa ufasaha ikiwemo kuwaelekeza wanafunzi na kufanya huduma ndogondogo inapotokea hitilafu katika vifaa husika.


 
Aliongeza kuwa manunuzi ya vifaa vya TEHAMA yamezingatia mwongozo wa SEQUIP ( ICT package) kwa kila Shule ya Sekondari inayonufaika. Kufuatia mwongozo huo vifaa vilivyonunuliwa ni  Kompyuta za mezani 1,848, UPS 462, Kompyuta Mpakato 231, Projekta 231 na Projekta “screen” 231

/ Published posts: 1594

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram