Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini makubaliano na Serikali ya Jamhuri ya Korea kusini kwa ajili ya ujenzi wa mradi mfumo wa uchakataji maji taka Mko wa Dar es salaam mradi utakaotumia zaidi ya dola za marekani milioni 90
Akizungumza leo Disemba 16, 2024 jijini Dar es salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano hayo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema tukio hilo ni matokeo ya ziara ya Rais Dkt Samia kutembelea Korea Kusini ambapo amesema mradi huo utakaotekelezwa kwenye wilaya za Kinondoni na Ilala utatekelezwa kwa miezi 36
Waziri Awesu ametumia mkutano huo kuwataka watendaji wa DAWASA kuhakikiaha wananchi wa Mkoa huo wanapata maji safi na salama bila kuleta visingizio kwani kwa sasa maji yapo
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo amezungumzia changamoto ya mtandao wa maji kutofika kwenye baadhi ya maeneo huku akiomba kupungua kwa muda wa mgao wa maji na kumaliza changamoto ya mfumo wa maji taka
Aidha naye Mtendaji mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire amesema mradi huo wenye thamani ya dola milioni 90 kutoka Korea kusini kupitia benki ya Exim ujenzi wake utatumia muda wa miezi 36 lengo likiwa ni kukabiliana na kiwango kikubwa cha maji yanayozalishwa.
Naye Balozi wq Korea kusini nchini Tanzania Ann Ewunju ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kwamba mradi huo unakwenda kutekelezwa kwa ubora na utakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa