Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
ADC Limited Tanzania Kwa kushirikiana na Equity Bank wamefanya semina ya kuwafunza wajasiriamali wanawake Kwa kuwapa elimu ya fedha na Uwekezaji na kuweka Bajeti na kujitenganisha na biashara zao
Hayo ameyasema Leo na Meneja wa wanawake na vijana kutoka Equity Bank Jackline Jacob Temu Amesema Equity Bank waliazisha dirisha la wanawake mwaka huu mwezi huu wa 5,”tunaelewa maitaji ya wanawake ni Zaidi ya pesa na Kuna wanawake wanapesa lakini wanachangamoto”.
“Sisi kama Equity Bank tuko Kwa ajili ya kuhakikishaย wanawake zile pesa tunazowapatia wanafanyia mambo ya maendeleo Kwa kukuza biashara zao Kwa sababu watu wengi wakipata pesa Kwa kuwa hawakuwa na elimu ya pesa wanajikuta wanaingia Kwenye madeni badala ya zileย pesa kuwasaidia unakuta zinawaletea matatizo”.Amesema Temu
Aidha amefafanua kuwa tunawapa elimu ya fedha na Uwekezaji na namna Gani ya kuweka malengo na Bajeti na kujitenganisha wao na biashara zao namna Gani wanaweza kusogea kutoka kwenda sehemu nyingine Kupitia Katika biashara walizokuwa nazo hayo yote yanafanyika na Equity Bank ikiwa kama eneo la Kuendelea kuwasitizia wanawake waendelee kukua kiuchumi.
Awali mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ADC Esta Kikota Amesema Mafunzo ambayo yanayotolewa niย Kwa wajasiriamali na pamoja naย kuwasapoti Yale yanayoelekezwa Katika kuhakikisha kwamba wanafikia vile vigezo vya kupata mikopo Kwa Kupitia dawati la wanamke plus ambalo limeazishwa rasmi Kwa ajili ya Biashara za wanawake.
Amesema katika program hiyo watafundisha mambo mbalimbali, program hiyo Iliyotengeneza Kwa kiasi kwamba Kwa kufikia vigezo vya kupata mikopo na sio kupata mikopo pekee yake maana unaweza kupata mkopo na ukashindwa kulipa na tunachoangalia Zaidi biashara zinakuwa na kuwa endelevu Kwa kuziendeleza Kwa vizazi na vizazi
“Kuna upungufu mkubwa sana wa mabank Kwa kutoa mikopo Kwa wajasiriamali wadogo na wakati hasa wanawake na Kwa Tanzania ukiangalia Kwa asilimia 90 za biashara zipo katika saizi biashara ndogo za kati lakini mchango Katika Pato la Taifa ni Katika asalimia kati ya 27 mpka 35 mchango wao ni mkubwa Kwa kuchangia Pato la Taifa”.Amesema Kikota
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Cotre Cotreda kinyaruki Amesema sisi kama wafanyabiashara tukikaa peke yetu tunaweza kufikili kuwa tunaelewa kumbe Kuna maeneo ambayo tunapata vikwazo mbalimbali lakini tukikaa na wataalumu Hawa wanakuwa wanafani mbalimbali za kutusaidia wanatuwezesha.
“Leo tumekuwa na somo zuri la utawala wa fedha Kwa kusimamia mradi kuwa na mpango wa kimkakati wa mpango wa kibiashara na sio kujiendea tu na matumizi mazuri ya pesa kuwa tunaitumiaje”.Amesema Kinyaruki
Halikadhalika nae Meneja wa Mafunzo ya Equity Bank Martin Rajabu Amesema kuwa Tumeazisha program maalumu Kwa ajili ya Mafunzo Kwa ajili ya elimu ya fedha na biashara ambayo ni Mafunzo ya vitendo na program ya Mwaka mzima
Katika utafiti uliofanyika wafanyabiashara wengi sana wamekuwa wanakosa elimu ya fedha na elimu sahihi ya Biashara tumeshazoea Katika taasisi nyingi za fedha,mashirika mengi yamekuwa yakiendesha semina ya Biashara na semina nyingi zimekuwa wakifanya semina Kwa siku Moja lakini Kwa uhalisia Kwa mtu uwezi kujua biashara A,Z Kwa siku Moja