Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba alizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Desemba 04, 2024 mkoani Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.
Jaji Warioba awataka vyama vya upinzani kuacha malalamiko dhidi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani ni dhahili kwamba hawakuwa na mpango madhubuti wa kuingia katika chaguzi hizo.
โHaya matatizo tuliyo nayo, kwa viwango vikubwa, yalitokana na awamu ya tano. Rais Samia alipoingia, alirithi yale matatizo. Lakini alikuwa na uthubutu wa kufanya maabdiliko. Yeye ndiye aliyeanzisha yale mazungumzo kati ya CCM na vyama vingine ili tufikie muafaka, mpaka akaleta 4R. Haikuwa kazi rahisi, lakini akaweza kukubaliana na ushauri,โWaziri Mkuu mstaafu Jaji Sinde Warioba.