106 views 2 mins 0 comments

VIJANA WA ACTION ROLLERS MTAA KWA MTAA KUTANGAZA KAMPENI YA UTALII KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU.

In KITAIFA
December 06, 2024

Na Kassim Nyaki NCAA



Kufuatia Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kuzindua msimu ya kampeni ya kuhamasisha utalii kwa wananchi kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka vijana wa Action Rollers Skates wako katika mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha kutangaza kampeni hiyo.

Vijana hao ni sehemu ya njia mbalimbali zinazotumiwa na NCAA kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa kutumia mabango yenye vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, kutembea na mabango yenye vifurushi vya gharama za kuingia hifadhini na kuvaa sare zaย  tisheti zenye ujumbe wa kuhamasisha kampeni hiyo kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kauli mbiu ya kampeni hiyo ni Merry and Wild; Ngorongoro Awaitsโ€ ambayo imeanza tarehe 4 Desemba, 2024 hadi tarehe 4 Januari, 2025 imegawanyika katika vifurushi vya aina tatu kama ifuatavyo;

Kifurushi cha FARU chenye gharama ya Shilingi 450,000 kwa mtu, ambapo gharama hiyo inahusisha utalii kwa siku mbili (02) hifadhi ya Ngorongoro, kiingilio, Malazi, Chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha na ambapo safari itakuwa tarehe 24-25 Desembaa 2024.

Kifurushi cha Pili ni TEMBO chenye gharama ya Shilingi 130,000 kwa mtu, kifurushi hiki kinahusisha utalii kwa siku moja (01) Day trip Ngorongoro na gharama hizo zitajumuisha kiingilio, chakula, muongoza watalii, Usafiri na huduma ya picha ambapo safari itakuwa tarehe 25 desemba, 2024

Kifurushi cha tatu ni CHUI chenye gharama yaย  Shilingi 85,000 kwa mtu na gharama hiyo itajumuisha Usafiri wa basi, kiingilio, Chakula, muongoza watalii na huduma ya picha ambapo safari tarehe 29 Desemba, 2024.

Katika utekelezaji wa Kampeni hiyo NCAA inashirikiana na kampuni ya _Tanzania Smile Safaris_ ambapo watanzania wanaopenda kunufaika na kampeni hiyo wanakaribishwa kupiga simu kwa namba 0755 559013 ili kuwekaย  nafasi (booking).

/ Published posts: 1588

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram