Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Ngome ya Vijana ya ACT Wazalendo kupitia kwa Naibu Katibu Vijana Taifa, Ruqayya Nassir leo tarehe 2 December 2024, Jijini Dar es Salaam ametoa rai kwa vijana nchini kupinga dhulma zote zinazolenga kuizika Demokrasia na kuzika matumaini ya kurejeshwa demokrasia ya kisiasa nchini.
Ruqayya amesema kwenye masuala haya ya kutekwa na kuumizwa kwa Viongozi wa Kisiasa taifa linapaswa kuwa pamoja, Pia amesema vijana wanapaswa kutoa dira na mwongozo kwa kuwa wao ndiyo wahanga wa utekaji unaoendelea.
Katika taarifa yake amelitaka Jeshi la Polisi kuwarudisha salama watu wate waliotekwa na kukomesha matukio ya uvunjifu wa haki yanayoendelea hakomeshwe mara moja.