Na Madina Mohammed ARUSHA
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassan Ameunda tume mbili Ambapo Moja atachunguza na kutoa mapendekezo Kuhusu maswala ya ardhi wanayolalamikiwa na wakazi wa ngorongoro.Tume nyengine itaangalia utekelezaji wa zoezi zima la uhamiaji wa hiari kutoka eneo la ngorongoro.
Dkt Samia ameyasema Leo ikulu ndogo ya Arusha wakati akizungumza na viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai (Malaigwanani) wanaoishi Katika eneo la ngorongoro.
Mkutano huo umefanyika Kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao Kwa kufuatia kuwepo Kwa malalamiko dhidi ya baadhi ya maamuzi wa serikali yanayohusu eneo la ngorongoro.
Rais Dkt Samia amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa mamlaka ya hifadhi ya eneo la ngorongoro NCAA Kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya serikali na jamii hiyo.
Vilevile amesisitiza ulazima wa wananchi kushirikishwa ipasavyo Katika upangaji na utekelezaji miradi inayopita kwenye maeneo Yao
Aidha Rais Dkt Samia amewasisitiza kuwa Tanzania ni nchi inayojivunia umoja wa kitaifa na yenye serikali inatowahudumia watanzania wote.
Hivyo ameitaka ofisi ya Rais Tamisemi kushughulikia changamoto zinazojitokeza ikiwemo kukosekana Kwa baadhi ya huduma za msingi na kijamii Katika eneo la ngorongoro.