7 views 55 secs 0 comments

KAPINGA ATUMIA FAINALI YA MPIRA WA MIGUU KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

In KITAIFA
November 25, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Asema baada ya michezo nguvu zielekezwe Novemba 27, 2024*

Awataka kuchagua viongozi makini wenye uchungu na maendeleo*

Asema CCM ndiyo chaguo SAHIHI*

Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ameendelea na kazi ya kuhamasisha Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma ili waweze kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.



Akiwa mgeni rasmi katika Fainali ya Mpira wa Miguu Mashindano ya Mkuu Super Cup katika Kata ya Matiri wilayani Mbinga, Kapinga amehamasisha makundi mbalimbali ya wananchi kushiriki katika uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa utakaofanyika nchi nzima.



” Ndugu zangu, wote tunafahamu kazi kubwa iliyopo mbele yetu ya kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi makini watakaokuwa wasimamizi wa shughuli za maendeleo katika maeneo yetu, kama ambavyo mmejitokeza kwa wingi katika fainali hii,ย  nguvu hii pia tuielekeze tarehe 27 Novemba 2024, siku ya kupiga kura.” Amesisitiza Kapinga



Kapinga ameendelea kuwakumbushaย  wananchiย  kuchagua Viongozi imara, makini na wenye uchungu na maendeleo katika maeneo yao huku akiweka mkazo kuwa Viongozi hao wanatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM).



Fainali ya Mkuu Super Cup ilihusishaย  timu ya Bodaboda FC na Afya FC ambapo Bodaboda FC iliibugiza timu ya Afya kwa goli 3, huku Afya ikiambulia goli moja.

Timu zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika michuano hiyo zimepata zawadi ikiwa ni njia ya kutoa motisha kwa vijana kujihusisha na michezo.

/ Published posts: 1500

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram