22 views 57 secs 0 comments

TRA,ZBS YAINGIA MAKUBALIANO KWENYE KURAHISISHA BIASHARA KATIKA FORODHA

In BIASHARA
November 06, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Mamlaka ya Mapato Nchini Tanzania( TRA) kwa kushirikiana na Shirika la viwango Zanzibar (SBZ) imesaini hati za makubaliano katika kwenda kurahisisha ufanyaji wa  biashara kwa pamoja.

Hayo yamesemwa Jijini Dar e salaam na Kamishina Mkuu wa mamlaka ya mapato nchini Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema kuwa TRA inasimamia shughuli za forodha kutoka bara hadi Zanzibar hivyo inaenda kurahisisha  mifumo ambayo inatumia forodha Zanzibar.



Katika makubaliano haya tunaenda kushirikiana  kwa kubadilishana Taarifa mbalimbali kwa kutumia mifumo huku mifumo ya ZBS ikiunganishwa na mifumo yetu kabla ya
kuruhusu mizigo itoke kwenye Bandari ya Zanzibar.

Aidha Kamishina Mwenda Aliongeza kuwa   kabla ya kuruhusu mizigo kutoka kwenye bandari ya Zanzibar itakaguliwa  na iwe imekidhi viwango huku taarifa mbalimbali zikiwemo ili kwenda kukuza na kuendeleza  biashara.

“Kupitia makubaliano haya tunaenda kupunguza Changamoto ya mizigo bandarini ambayo ilikuwa inapitia bandari ya zanzibar Pia niwahakikishie wafanyabiashara wa bandari kutoka Zanzibar TRA na ZBS  zimekuwa karibu na itaenda kurahisisha ukaguzi wa mizigo inayopita Bandari ya Zanzibar ” Amesema Kamishina Mwenda



Naye  Mkurugenzi kutoka Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) Yusuph Nassor Ameongeza kuwa mapato ambayo tunapata ZBS ni kutokana na ushirikiano kutoka TRA hivyo tunapata mchango mkubwa na kuweza kuimarisha mifumo yetu kwa pamoja kupitia utendaji kazi.

Kwa upande wetu Zanzibar tunataka tusitoe huduma kwa mtu yeyote ambaye hajasajiliwa na TIN namba hivyo tunaenda kuhakikisha tunaingiza mizigo kwa upande wa zanzibar kwa mfanyabiashara Mjasiriamali, au mwenye kiwanda anatakiwa kukaguliwa na TRA

/ Published posts: 1488

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram