24 views 4 mins 0 comments

KAMISHNA TRA ATIMIZA SIKU 100 AKIAINISHA MAMBO 10

In BIASHARA
October 28, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Aeleza mkakati wa kuongeza wigo ukusanyaj nchini, amshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumuamini


DAR ES SALAAM

KAMISHNA mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda ameelezzea siku 100 za utumishi wake katika nafasi hiyo huku akisisitiza kuwa mamlaka hiyo inaamini katika kuwa na ushirikiano bora na uhusiano imara na walipa kodi bila ya kuhatarisha ulipaji kodi stahiki kwa mujibu wa sheria.

Katika andiko lake la kushukuru aliloliweka katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook Mwenda alisema kuwa anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kibali cha kutimiza siku 100, akiwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), baada ya kuaminiwa na kuapishwa na Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan.

“Aidha namshukuru sana Mheshimiwa Rais, kuendelea kuniamini kumsaidia kusimamia uendeshaji wa TRA,Pia nawashukuru viongozi wote wa Serikali, Wananchi na Walipakodi wote, Mwenyekiti na bodi ya Wakurugenzi ya TRA, pamoja na Watumishi Wote wa TRA kwa Ushirikiano  mkubwa wanaonipa katika kipindi cha siku 100.

“Kwa pamoja tumethibitisha kwamba tunaweza  kuwa na Ushirikiano na Uhusiano mzuri kati ya TRA na Walipakodi bila ya Kuhatarisha Ulipaji Kodi Stahiki Kwa mujibu wa sheria  kama tulivyofanya,” alisema Mwenda

Aidha, aliongeza kuwa wanaweza kuongeza makusanyo ya Kodi bila ya migogoro na walipakodi, kama ilivyowezekana katika  Makusanyo ya robo mwaka ya kwanza ya ( Julai – Sept, 2024) kwa kuongeza asilimia 18 ya makusanyo ya kodi.

Mwenda ambaye kabla ya kuwa Kamishna Mkuu wa TRA alikuwa Kamishna wa mamlakaa ya kodi Zanzibar (ZRA),katika aandiko lake hilo la mtandaoni ameongeza kuwa wanaweza kuwatembelea na kuwasikiliza walipakodi wa nchi  nzima .

“Kama tulivyotembelea mikoa 25 nchi nzima ili kuwasikiliza, kutatua migogoro yao ya kikodi kwa wakati pamoja na  kuwa Wabunifu wa kutumia mifumo rahisi ya kuwasikiliza ili kupata mrejesho toka kwa wananchi na walipakodi Wote.

“Tunaweza kuwekeza na kuharakisha ujenzi wa Mifumo ya Usimamizi wa Kodi ya IDRAS na TANCIS ambayo inasomana na mifumo mingine ili kurahisisha zaidi ulipaji na ongezeko la kodi, pia tunaweza kujenga Mifumo ya kusimamia Bandari zetu na mipaka yetu vizuri, na kuweka mazingira ya ushindani yaliyo sawa ili kuwezesha biashara na makusanyo ya kodi ya forodha kuongezeka,” alisema



Akiendelea kuelezea mafanikio ya siku 100 katika nafaasi hiyo Mwenda amesema wanaweza kuimarisha huduma za Kodi pamoja na  matumizi sahihi ya mfumo wa EFD na kuchukua hatua kwa wasiotumia  kwa mujibu na  kutumia Sheria za Kodi, mifumo ya usimamizi wa kodi( EFDMS) na ushirikiswaji wa walipakodi.

Ametumia maadhimisho hayo ya siku 100 kazini kueleza kuwa wanaweza  Kuendelea  Kutoa Elimu ya Kodi kwa njia tofauti zenye  tija  na zinazoleta matokeo Chanya ikiwemo  kuimarisha Ukaguzi na uchunguzi ili kuwatambua na kuwachukulia hatua wachache waepa na wakwepa kodi ili kuleta usawa katika shughuli za kiuchumi nchini.

“Tunaweza kama TRA kuendelea kuongeza idadi ya walipakodi nchini, kuimarisha utoaji wa huduma nzuri, kuongeza Uweledi, Ubunifu na Uadilifu,pamoja na kuwajali wateja wetu ili kuimarisha ulipaji Kodi wa hiari nchini.

Alisisitiza kuwa TRA itaendelea kushirikiana na wadau wote wa kodi, wakiwemo Viongozi wa taasisi na Jumuiya za Wafanyabiashara nchini ili kuendelea kujenga na kuimarisha Mfumo wa kodi ulio sawa, unaoabirika, unaowezesha ukuaji wa biashara nchini, wenye ufanisi, unaowezesha utatuzi wa migogoro ya kikodi kwa haraka na unaohamasisha wananchi na wafanyabiashara kufurahia kulipa kodi kwa hiari.

Akitumia kauli mbiu ya Pamoja tunajenga Taifa Mwernda amewashukuru   walipakodi wote na kuwahakikishia, TRA, itaendelea kutekeleza maagizo yote Rais Dkt Samia  ya kuwasikiliza walipakodi, kuendelea kutoa elimu ya kodi, kuweka mazingira wezeshi ya  shughuli za Kiuchumi nchini, kuimarisha utoaji wa huduma za kodi  na Kuendelea kufanya vizuri zaidi ili kuiwezesha Serikali kutimiza majukumu yake ya kuwaletea maendeleo wananchi.

/ Published posts: 1450

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram