126 views 10 secs 0 comments

TANGA: MAFANIKIO YA MABORESHO BANDARI YA TANGA

In KITAIFA
October 22, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Katika Kipindi cha Miezi mitatu ya robo mwaka wa fedha 2024/2025 bandari ya Tanga ilipangiwa kukusanya mapato kiasi cha Shilingi bilioni 11 ambapo mpaka mwezi September wamevuka lengo na kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 18.6.

Mafanikio ya Maboresho ya bandari ya Tanga yanaendelea kuonekana kutokana na ongezeko la Meli zinazoitumia bandari hiyo hatua ambayo inawarahisishia wafanyabiashara kupata huduma kwa haraka.

Akizungumzia manufaa yaliyotokana na maboresho hayo Meneja wa bandari ya Tanga MASOUD MRISHA amesema hatua hiyo ni pamoja na kuwepo kwa mazingira yanayowezesha kupita kwa bidhaa ambazo awali hazikuwahi kupita bandarini hapa.



Katika hatua nyingine meli kubwa kutoka nchini China imetia nanga bandarini hapo ikiwa na shehena mbalimbali yakiwemo magari zaidi ya 350 na hapa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA ENOCK BWIGANE anaeleza namna wanavyohudumia shehena za mizigo kwa kipindi kifupi.

/ Published posts: 1614

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram