76 views 2 mins 0 comments

WAZIRI MBARAWA: SERIKALI INATARAJIA KUTUMIA SH BILIONI 600 KUGHARAMIA MIRADI 3

In KITAIFA
October 17, 2024

Na MADINA MOHAMMED WAMACHINGA


Serikali inatarajia kutumia Shilingi Bilioni 600 kwa ajili ya kugharamia Miradi mitatu  itakayoboresha huduma ya usafirishaji kwa njia ya maji mkoani Kigoma  na maeneo yanayozunguka.

Akizungumza  wakati wa kufungua  mkutano wa pili wa kimataifa wa lojistiki na Uchukuzi,Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa  amesema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha meli,ujenzi wa meli ya mizigo pamoja na ujenzi wa meli ya kisasa ya abiria  inayotarajiwa kufanya safari zake katika ziwa Tanganyika pamoja na Ziwa Victoria.

“Bandari ya Kigoma ni bandari muhimu kwa sababu kwenye ziwa Tanganyika tunapakana na DRC  na kule kuna madini,Kigoma ni karibu  sana na Congo,kutokana na hilo serikali tukaona tuweke nguvu zakutosha  kuhakikisha tunatumia bandari ya Kigoma ipasavyo kujenga vyombo vya kisasa,”amesema Mbarawa.



Amesema kiwanda cha meli kinategemewa kujenga meli za kisasa huku ujenzi wa meli ya kisasa ya abiria inayotarajiwa kubeba kati ya abiria 600 mpaka 900 na meli ya mizigo inayotarajiwa kubeba tani 3000 za mizigo ambapo itakuwa pia na njia za magari kwa mfumo wa mlango kwa mlango.

“Miradi hii yote ambayo itaanza hivi karibuni  itagharimu Sh Bilioni 600 ambapo itaboresha suala la usafirishaji katika bandari ya Kigoma,”amesema Profesa Mbarawa

Amesema kuna maendeleo mbalimbali yanaenda  kwa kasi kubwa,usafiri wa reli na majini ambapo kukamilika wa miradi hiyo kutaleta  ajira  kufungua sekta ya usafirishaji,kuleta ajira na kukuza uchumi,”amesema Profesa Mbarawa



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chuo  Cha Usafirishaji (NIT)  Profesa Ulingeta Mbamba amesema  serikali imeandaa mkutano huu kwa ajili ya kuwakutanisha wataalam  wajadili kwa kiasi gani nchi inaweza kupiga  hatua kwa kufanya tafiti katika Usafirishaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha NIT Dk.Prosper Mgaya  amesema kongamano hilo la siku tatu litajadili mambo  mbalimbali ambapo kutakuwa na mawasilisho kutoka kwa wataalamu wa masuala ya usafirishaji.

/ Published posts: 1458

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram