43 views 2 mins 0 comments

MCHENGERWA AIBUKA HOJA YA VITUO BANDIA

In KITAIFA
October 16, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA



Asema hakuna vituo vya aina hiyo katika andikishaji wapiga kura, aweka wazi uandikishaji unafanyika kwenye vituo 80,812 nchini



-MWANZA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu uwepo wa vituo bandia vya kuandikisha wapigakura wa Serikali za Mitaa sio za kweli.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa taarifa sahihi ni kuwa alifafanua kuwa uandikishaji  unafanyika kwenye vituo 80,812 kutokana na kuwa kuna baadhi ya mitaa au vitongoji vina vituo zaidi ya kimoja.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 796 kuhusu orodha ya maeneo yatakayoshiki uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

“Ifahamike kuwa kwa Mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 796 na 797 kuhusu orodha ya maeneo yatakayoshiriki uchaguzi yanajumuisha jumla ya mitaa na vitongoji 68,543 lakini vituo vilivyopo ni 80,812 . Lengo la kuwa na vituo hivi ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa ili kupata haki yao ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa.

“Hii ina maana vipo vitongoji na mitaa ambayo inakituo zaidi ya kimoja na hii imefanyika miaka yote ya uchaguzi kutokana na wingi wa watu, jiogarafia ya mahali ya eneo husika mfano misitu au wananchi wana shughuli za kiuchumi katika maeneo ya wafugaji, wakulima, wachimbaji migodini au wananchi wanaishi mbali na kituo cha uandikishaji hivyo kwa pamoja wasimamizi na viongozi wa vyama wanakubalina kuongeza kituo ili kuwafikia wananchi wote,” alisema Mchengerwa

Aidha aliongeza kuwa kutowafikishia wananchi fursa ya kuwa na kituo ni kuwanyima haki yao ya kikatiba.



Waziri Mchengerwa alisema kuwa suala la msingi pale inapobainika uhitaji wa kituo cha kuandikisha na kupiga kura, Kanuni zinaelekeza vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi katika eneo husika kukubaliana na kuamua ni wapi kituo kiwekwe ili kuhakikisha wananchama wao na wananchi wengine wote wanapata fursa hii ya kikatiba pasipo na kikwazo.

Akifafanua hoja hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wadau wa uchaguzi hususan ni kipindi hiki cha uandikishaji, ambapo aliwataka wadau wa vyama pamoja na wasimamizi wa uchaguzi/wasimamizi wasaidizi kukubaliana maeneo yote ambayo ni muhimu kukawa na vituo kwa nia ya kuwafikia wananchi wote pasipo na vikwazo.

/ Published posts: 1450

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram