54 views 2 mins 0 comments

SAMIA FASHION FESTIVAL KUINUA WABUNIFU WA MAVAZI

In BURUDANI
October 12, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Muanzilishi na Mratibu wa Tamasha la Samia Festival Hadija Mwanamboka amesema tamasha hilo ni mahususi kwaajili ya kuinua wabunifu wa mavazi nchini Tanzania

Amesema hayo Octoba 11 Jijini Dar es salaam wakati wakitambulisha Tamasha hilo litakalo anza kufanyika Novemba 27 Jijini humo akieleza kuwa lengo kuu ni kuwapa jukwaa wabunifu kutengeneza mavazi yanayo landana na ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan



Amesema katika tamasha hilo wataanza kufanya maoneshi ya mavazi hayo watoto kuanzia miaka 9 hadi 17 ili kuwajengea uwezo na kuibua vipaji hata wakiwa katika umri mdogo pamoja na kutoa wito kwa wabunifu kushiriki ili kutangaza kazi zao na kuinua kipato.

Mwanamboka ameeleza kwamba tamasha hili limepewa jina kwa heshima ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na maono yake na ni heshima kwa uongozi wake katika kukuza utamaduni wa Tanzania kupitia mavazi hasa katika sekta ya ubunifu.



“Tamasha hili limepewa jina kwa heshima ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na limelenga kukuza utamaduni wa Tanzania kupitia mavazi Hulu likionyesha mchango wa Rais katika sekta ya ubunifu.Tamasha litaendelea kwa siku Saba,likijumuisha matukio mbalimbali ya kuwawezesha wanawake,watoto na vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar”,amesema

Aidha kauli mbiu ya tamasha hili ni”Ubunifu na Stara” ikiwa ni taswira tosha ya nafasi na haiba ya mama yeti mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na kwa jinsi Gani jamii inaweza kutumia haiba hiyo yenye stara katika nyanja mbalimbalo za kijamii kama vile motiko,sherehe ,shughuli za jioni ,malezi na kadhalika.



“Tamasha hili si sherehe ya mavazi tu, ni jukwaa la kuonyesha ubunifu wa Kitanzania na ni heshima kwa uongozi na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan “,amesema Khadija Mwanamboka .

Aliongeza kwamba anawakaribisha wabunifu wote kwa mikoa yote ya Tanzania kushiriki fursa hii kwa kutuma kazi zao na jopo la majajo mahiri na wazoefu katika sekta ya mitindo wakiongozwa na Chief Judge mwanamitindo Miriam Odemba ,Mwanamitindo wa Kitanzania anayeishi Ufaransa.

/ Published posts: 1450

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram