Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Jana oktoba 9,2024 Umoja wa Shirikisho la Wamachinga Tanzania SHIUMA umezindua mpango kazi (Operesheni ) ya kampeni ya “Mama Tuvushe 2025 “
Wamezindua mpango kazi huo (Operesheni )utakaofanyakazi nchi nzima kuzunguka kutokana na maadhimio ya kampeni hiyo,Yote hayo yamejiri wakati wa kikao chao walichokifanya leo mkoani Iringa mbele ya Wamachinga waliojitokeza hapo na viongozi mbalimbali wa Mkoa
*Ikumbukwe* kampeni hiyo ilizinduliwa Oktoba 21 mwaka 2023 ikiwa na lengo la kumuunga mkono Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na mchango wake kwa Wafanyabiashara hao
TUTAENDELEA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA HADI MWAKA 2025
SHIRIKISHO la umoja wa Wamachinga Tanzania (SHIUMA) limetangaza kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwasababu amewafikishia fursa mbalimbali za kimaendeleo katika umoja wao hivyo hawana budi kurejesha fadhila na mpango wao /kampeni itakayozungumzia kazi za Rais ” *Mama Tuvushe 2025* ” inaanza punde kuzunguka Tanzania nzima
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 9,2024 na Katibu mkuu Taifa wa umoja huo Ndg.Venatory Mgayane pamoja na naibu katibu wake mkuu Joseph Mwanakijiji mkoani Iringa katika mkutano wao na wanachama ambapo mgeni rasmi akiwa Ndg.Joseph Ryata Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapo.
Mgayane ametolea mfano wa mafanikio kuwa Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki utakaowasajili wamachinga, wakitoa vitambulisho maalum vitakavyowasaidia kupata mikopo kirahisi, bima za afya, na fursa za biashara. Aidha, amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya mikopo ya wamachinga, huku riba ikiwa imepunguzwa kutoka 10% hadi 7%.