35 views 52 secs 0 comments

KONGAMANO LA UTENGAMAO WA AKILI KUFANYIKA JNICC

In KITAIFA
September 11, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Rihab Health imeandaa Kongamano la pili la Utengamao wa akili (Rehabilitationย  summit) linalokusudia kuendeleza ajenda ya utengamao wa Afya ya akili nchini lenye kauli mbiu ya “kuendeleza ajenda ya utengamao,kuimarisha mifumo ya Afya nchini.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Remla Shirima amezungumza na waandishi wa habari leo septemba 11 jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwaย  kongamano hilo litawakutanisha watalam,watunga sera,watoa huduma za Afya ambapo watajadili mikakatiย  na kuvumbua mbinu bora za huduma kwa wagonjwa wa utengamao wa akili.

“Tunalenga kuimarisha mfumo wa afya Kwa kuhakikisha huduma za utengamao zinafika Katika ngazi za msingi.za huduma za Afya na jamii”.Amesema Shirika

Pia Ameongeza kuwa “tunataka kubadilisha maarifa Kuhusu utafiti wa hivi karibuni,uvumbuzi, na mbinu Bora za kuboresha huduma za utengamao Kwa wagonjwa”.

Aidha Shirima Amesema kongamano hilo litakuwa na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa masuala ya muhimu Kama Jinsi ya kuongeza upatikanaji wa huduma za utengamao Katika maeneo ya vijijini ana yenye uhaba WA rasilimali.

“Kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi Ili kuboresha miundombinu ya huduma za utengamao na kutoa mapendekezo muhimu ya kisera na hatua za kuboresha huduma za utengamao Nchini Tanzania”. Ameongeza Shirima



Ametoa wito kwa wadau wa afya na maendeleo kushiriki katika kogamano hilo la siku tatu linatarajiwa kufanyika kuanzia 18 na kumalizika 20 septemba mwaka huu .

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram