Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa suala la kuilinda nchi ni wajibu wa Watanzania wote kwa ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Majaliwa amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vina jukumu la kupokea taarifa mbalimbali zinazoonyesha uvunjifu wa amani popote pale .
Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Vitu Maalum, Mhe. Anatropia Theonest, aliyetaka kujua mikakati ya Serikali kuhusu matukio ya utekaji yanayoripotiwa kutokea nchini.
Aidha Majaliwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kujikita kusimamia misingi ya amani katika nchi.