Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) leo tarehe 21 Agosti 2024 atafungua Kongamano la tisa (9) la Wahandisi Wanawake nchini linalofanyika Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaam (JNICC).
Kongamano hilo linafanyika siku mbili kwa kuwakutanisha wanataaluma, wahandisi wanawake pamoja na wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi ambapo limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Said, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) na Wakuu wa Taasisi zinazohudumia Wahandisi.
Kongamano hilo linaongozwa na Kauli mbiu isemayo โHarnessing the Strength of Women Engineers to Drive Progress Towards a Sustainable Worldโ.