87 views 2 mins 0 comments

MAADHIMISHO YA SIKU YA HOMA YA INI KITAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM

In KITAIFA
July 26, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-RC Chalamila awataka wakazi wa Mkoa huo na watanzania kujitokeza kwa wingi

-Asema maadhimisho hayo yanaanza Julai 25 hadi 28,2024

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 25,2024 ametoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya Siku ya Homa ya INI ambayo yatafanyika katika viwanja vya Sinza Darajani Halmashauri ya Ubungo tarehe 25-28 Julai,2024 kuanzia saa 02:00 Asubuhi.

RC Chalamila amesema Mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya ngono na Homa ya INI pamoja na Halmashauri zake tano na wadau mbalimbali wa maendeleo watafanya maadhimisho ya siku ya Homa ya INI kitaifa ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika katika Mkoa huu.

Aidha RC Chalamila amesema maadhimisho hayo yanakusudia kutoa elimu na uelewa wa pamoja juu ya ugonjwa wa Homa ya INI pamoja na kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwemo huduma za Homa ya INI kama upimaji wa maambukizi ya virusi vya Homa ya INI, Chanjo za homa ya INI pamoja na huduma zingine za Afyaย  na magonjwa mengine.

Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa amesema katika kilele cha maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe Ummy Mwalimu (MB) Waziri wa Afya.

Mwisho RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji mkubwa anaoufanya katika sekta ya Afyaย  kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya na kwa Wakati โ€œ Nimalize kwa kusema ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mapambano ya Homa ya INI au Ni Wakati wa Vitendoโ€ Alisema Chalamila.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram