191 views 2 mins 0 comments

VIONGOZI WA ACT WAZALENDO WAMJIA JUU WAZIRI NAPE

In KITAIFA
July 17, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

Viongozi wakuu wa Chama cha ACT Wazalendo wanatarajia kufanya ziara ya kikazi kwenye mikoa 22 na majimbo 125 ya Tanzania Bara kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu (2024) na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani (2025)

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa mbele ya wanahabari leo, Jumatano Julai 17.2024 kupitia kwa Naibu Katibu wa Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na umma Shangwe Ayo imeeleza kuwa inatarajiwa kuanza Julai 22.2024 ambapo Kiongozi wa ACT Wazalendo Dorothy Semu atatembelea majimbo 30 kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida na Manyara, huku Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara Isihaka Mchinjita akitarajiwa kutembelea majimbo 38 kwenye mikoa ya Ruvuma, mkoa wa kichama wa Selous, Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga

Aidha, Shangwe Ayo ameeleza kuwa katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu atatembelea majimbo 21 kwenye mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera, wakati huohuo Kiongozi mstaafu wa chama hicho Zitto Kabwe atatembelea majimbo 36 kwenye mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, mkoa wa kichama Kahama na Shinyanga

Imeelezwa kuwa kupitia ziara hiyo chama hicho kinatarajia kuzindua mpango wa kusajili wanachama wapya milioni 10 ndani ya kipindi cha miezi 10 kuanzia mwezi Julai 2024 na Aprili 2025, sambamba na hilo viongozi hao wanatarajia kuwahamasisha Watanzania kujiandikisha kuwa wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa (2024) na uchaguzi mkuu (2025) wakilenga kuona chama hicho kinapata ushindi wa kishindo kwenye chaguzi hizo

Sambamba na hilo, viongozi wakuu wa ACT Wazalendo wanakusudia kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazohusu masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili wazipazie sauti na kuendelea kuinadi ahadi ya chama hicho kwa Watanzania ya kujenga ‘Taifa la wote, maslahi ya wote’.

/ Published posts: 1488

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram