Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Alhamis, 11 Julai 2024, amefungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wilaya zote na mikoa yote, nchi nzima, yanayofanyika katika Chuo cha UVCCM Ihemi, mkoani Iringa.
Baada ya kuwasili chuoni hapo, Balozi Nchimbi amepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Mohammed Ali Mohammed Kawaida pamoja na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Komredi Joketi Urban Mwegelo, ambapo pamoja na masuala mengine amewapongeza jinsi walivyozindua mkakati wao wa kuhamasisha vijana, *TUNAZIMA ZOTE, TUNAWASHA KIJANI*, kwa kishindo kikubwa kiasi cha kuweka rekodi mpya ya kuujaza Uwanja wa Mpira wa Benjamin William Mkapa, almaarufu Lupaso au kwa Mkapa.