Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Waziri wa Maji Juma Aweso amesema serikali kupitia Wizara ya Maji ipo kwenye mchakato wa kuweka luku ya maji ambayo itaenda kutatua tatizo la wananchi kupatiwa bili ambazo si sahihi kulingana na matumizi yao
Ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam akiwa katika ziara yake jijini humo ambapo amepata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa Wilaya ya Ilala kata ya Tabata Segerea na kusikiliza malalamiko na kero zao juu ya huduma hiyo muhimu kwa lengo la kuboresha huduma ya maji Tabata.
โNataka niwape salamu za Rais Samia Suluhu Hassan ndugu zangu wanasegerea hii changamoto tumeiona Wizara ya Maji tumeelekezwa na Rais tunakwenda kuweka luku ya maji tunatumia kama umeme, maswala ya kubambikizia wananchi bili ya maji wasoma mita hizo zilipendwa dunia ya sasa haiwezekani tuendelee katika mwenendo huo tunakupa mita ya luku unanunua maji yako ya elfu tano unayatumia yanaishaโ Aweso
Aidha, amewapiga marufuku DAWASA kumbambikizia mwananchi bili ya maji na kuwataka kutoza fedha ya maji kutokana na matumizi sahihi ya muhusika.
โNi marufuku kumbambikizia mwananchi bili za maji kuna jambo nataka nizungumze jambo la kwanza, msoma mita anapoenda kusoma mita kwa mwananchi lazima amshirikishe, msoma mita unapoenda kusoma mita usikadirie usije ukasema huyu mama anatumiaga kwenye elfu 50 ngoja nimuwekee elfu 70 haiwezekani, mara nyingine msoma mita anaweza asifike eneo la nyumba husika akaandika laki na nusu aseme huyu dada si anaongea kwenye mkutano piga laki na sitini haiwezekaniโ Aweso